HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 6, 2020

DKT TULIA APEWA ULEZI WA WATOTO WA KITUO CHA JERUSALEM KIMARA KKKT

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson leo amepewa kuwa mama mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Jerusalem kinachosimamiwa na kanisa la KKKT Kimara. 
 
Akizungumza katika ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Kimara jijini Dar es Salaam, Mchungaji Kiongozi, Wilbrod Mastai amesema kuwa mbali na Mheshimiwa Dkt Tulia kuwa mlezi wa kituo hicho wameamua kumpa kuwa mzazi wa hao watoto. 
 
"Tumeamua kumpa heshima ya pekee ya kuwa mzazi wa watoto 21 wa kituo chetu cha kulelea watoto Yatima kinachosimamiwa na kanisa letu, hivyo tunamshukuru kwa kuweza kukubali ombi letu," amesema. 
 
Katika tukio lililovuta hisia za waumini ni kubatizwa kwa mtoto mmoja kati ya hao 21 Meshack Elinaza ambaye anawiki mbili tokea amepokelewa kituoni hapo.
 
 Kwa upande wa Dkt Tulia Ackson ameshukuru uongozi wa kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Kimara kwa kuweza kumpa heshima ya kuwa mama wa watoto hao, huku akiahidi kuwalea katika maadili ya kidini na kuweza kumjua Mungu. 
 
"Niwashukuru kwa kunipa heshima ya pekee kwasasa nitakuwa nanyi bega kwa bega katika kuwalea watoto hawa waliopo kituo chenu, sina mengi zaidi kuzidi kushukuru na mzidi kuniombea ili niweze kuwa mama bora," amesema Dkt Tulia Ackson.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson akisimamia ubatizo wa Mtoto Meshack Elinaza anayelelewa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Jerusalem kinachosimamiwa na kanisa la KKKT Kimara, ambacho Dkt. Tulia ndiye mlezi wake. anayembatiza Mtoto huyo ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) - Kimara, Wilbrod Mastai.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson akizungumza na waumini wa kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) - Kimara,wakati alipata nafasi ya kuzungumza nao baada ya Ibada ya Jumapili.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) - Kimara, Wilbrod Mastai akitoa mahubiri kwa waumini wa kanisa hilo.
Sehemu ya Viongozi walioshiriki Ibada hiyo ya Jumalipi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad