BODI YA KOROSHO, SERIKALI KUCHUNGUZA WANAOHUJUMU SOKO LA KOROSHO WILAYANI TANDAHIMBA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 14, 2020

BODI YA KOROSHO, SERIKALI KUCHUNGUZA WANAOHUJUMU SOKO LA KOROSHO WILAYANI TANDAHIMBA

 

Na Mwaandishi Wetu Mtwara.

CHAMA cha Ushirika cha Tandahimba Newala (TANECU)kimeomba bodi ya korosho ikiongozwa na Serikali ya Wilaya ya Tandahimba kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria kwa watu ambao wanalengo la kuhujumu soko la korosho wilayani humo.

Akizungumza leo, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Shaibu Njauka ametoa rai hiyo baada ya wanunuzi wa korosho kukataa kununua korosho tani 710 kwa madai korosho hizo zina unyevunyevu.


Kutokana na malalamiko hayo, Bodi ya Korosho ilituma wataalum wake kufanya ukaguzi wa kuhakiki madai hayo na kueleza korosho hizo za daraja la kwanza ni  nzuri na hazikuwa tatizo hilo.

Akizungumzia hatua hiyo ya wanunuzi kuzikataa korosho na baada ya matokea kuonesha hazikuwa na tatizo, Njauka amesema wanunuzi hao wana nia ya kutaka kununua korosho hizo kwa bei ya chini ambayo inakuwa ni hasara kwa mkulima.

"Tuliwaomba watu wa bodi ya korosho waje waangalie ubora unaolalamikiwa na wafanyabishara katika ghala la tandahimba, Mungu ni mwena, watu wa bodi ya korosho Wamefanya jukumu lao na wamejiridhisha, kwamba korosho za Tandahimba hazina tatizo ni za daraja la kwanza unyevu upo 9.4 na ‘outturn’ iko kati ya 49-51,"amesema.

Njauka amesema ni vitu vya kushangaza kwa baadhi ya wanunuzi kuleta propaganda kwenye ghala la Tandahimba huku akiwata bodi ya na Serikali ya wilaya kufanya uchunguzi kwa watu ambao wana lengo la kuhujumu Tandahimba.

"Kwa sababu kama uchunguzi umoenesha korosho ni daraja la kwanza tatizo la wanunuzi kuzitaka korosho linatoka wapi, kama kuna uwezekana kwa hao wanunuzi ku-doubt kama sisi korosho zetu ni za daraja la chini basi ni vizuri waitwe ili watoe uthibitishi na kama hawatakuwa na uthibitisho basi miongozi iko wazi, bodi ya korosho ichukue hatua," amesema.

Baada ya bodi kuthibitisha kuwa korosho hizo ziko katika hali nzuri na ni za daraja la kwanza, chama hicho kiliuza korosho tani 5394 zikiwemo tani 710 zilizokataliwa na wanunuzi kwenye mnada uliopita kwa madai kwamba korosho hizo zilikuwa na unyevu.

Korosho hizo ziliuzwa kwenye mnada wa kumi  wa mauzo uliofanyika wilayani Newala wiki iliyopita zote zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi billion 11.6 huku bei ya juu kilo moja ikiuzwa kwa shiling 2307 na bei ya chini ikiwa ni shilingi 2100.

Akizungumza katika mnada Njauka amesema  bei hizo za korosho zinatokana na wanunuzi wa zao hilo kupungua. "Bei kubwa ya korosho ilikuwa ni  shilingi 2307 huku bei ya chini ikiwa ni Sh.2,100 bei ambayo wakulima wameridhia kuuza na korosho zote zilikuwa kwenye ghala ya wilaya ya Tandahimba na Newala," amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho (CBT) Alfredy Francis aliyeudhuria mnada huo amewataka wakulima kuendelea kuhifadhi korosho katika mazingira bora ili ziweze kununulika na kupata bei nzuri kwa wanunuzi.

Amesema vipo baadhi ya vyama vya ushirika vinaendelea kupokea korosho chafu kutoka kwa wakulima wasio waadilifu na hivyo kuhatarisha kushusha  thamani ya zao hilo.

Makamu Mwenyekiti wa TANECU Shaibu Njauka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad