Balozi
wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab alikutana na Shirika la
Qatar Travel Mart (QTM) linalojishughulisha kutangaza utalii wa ndani na
nje ya Qatar pamoja na kuandaa Maonesho ya Utalii. Shirika hilo
linajiandaa kufanya Maonesho Makubwa ya Utalii yatakayofanyika tarehe
17-19 November 2021. Mataifa mengi ya kigeni ya Asia, Ulaya na Marekani
yanatarajiwa kushiriki Maonesho hayo pamoja na ofisi za Kibalozi ziliopo
Qatar.
Maonesho hayo yatatoa fursa kwa nchi kutangaza Biashara, uwekezaji na
Sanaa. Mhe. Balozi amewaahidi kuwa Tanzania itashiriki kikamilifu kwenye
Maonesho hayo. Aidha kabla ya Maonesho hayo Ubalozi utaandaa Mkutano wa
Mtandao Webinar Conference mwezi Desemba 2020 baina ya Shirika hilo la
QTM na TTB na ZTC ili kuelezea vivutio vya Utalii vya Tanzania na
kukaribisha watalii kutoka Qatar
Wednesday, October 14, 2020

Tanzania Kutumia Maonesho Makubwa ya Qatar Kutangaza Utalii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment