STEMM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MIFUPA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 16, 2020

STEMM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MIFUPA

 

Dr. Steve Meyer akiwa na Dr bingwa wa mifupa kutoka hospitali ya Mount Meru Dr Elias Mashalla na mjumbe wabodi ya stemm na mgombea ubunge jimbo la Arumeru magharibi kwenye kontena lenye vifaa vya mifupa liko katika kituo cha watoto yatima Cha stemm,Mbuguni
Wa kwanza kushoto ni mke wa Dr Steve Meyer,wa pili Dr Steve Meyer ,akifuatiwa na mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dr focus Maneno.


Na.Vero Ignatus.
Shirika lisilo la Kiserikali la Stemm linalojishughukisha na Elimu,Afya na watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi limekabidhi vifaa vya upasuaji wa mifupa na afya vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 kwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Arumeru, mkoani Arusha.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo DR,STEVEN MEYER katika kituo cha watoto yatima kilichopo kijiji cha Kikuletwa , kata ya mbuguni ,wilaya Arumeru, amesema lengo la msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi watatu walionusurika katika ajali iliyohusisha gari la shule ya msingi Luck vincent iliyotokea mwezi meii mwaka 2017, na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, waalimu 2 na dereva 1 eneo la Rotia wilaya ya Karatu.

Hata hivyo amesema kuwa vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa hospitali za mkoa wa Arusha pindi wagonjwa watakapohitaji matibabu ya mifupa; huku akimshukuru Rais Dr,John Magufuli kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya afya hasa kufanikisha upatikanaji wa hati za kusafiria manusura wanafunzi wa ajali hiyo ambao ni Doreen ,Elibariki,Sadia Awadh na Wilson Godfrey ambapo kwa sasa wanasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Star High School .

Akipokea msaada huo Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dr, Focus Maneno alimesema kuwa umekuja wakati muafaka ambapo hospitali hizo zinahitaji vifaa hivyo kwa matibabu ya wagonjwa wa mifupa.

Amesema kuwa licha ya msaada huo bado wanakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa wa mifupa ambapo inawalazimu kuwapa rufaa kwenda kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Stemm ambae pia ni mgombea Ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Dr.John Palangyo kwa niaba ya wanachi wilaya ya Arumeru ameshukuru kwa vifaa hivyo ambavyo vitakuwa msaada mkubwa hasa kipindi hiki ambapo watanzania wanahitaji zaidi huduma za afya ya mifupa na kupunguza gharama za kutibiwa nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kikuletwa Hosea Palangyo amelishukuru Shirika hilo kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani wananchi walikuwa wanatumia gharama kubwa kufuata matibabu ya mifupa nje ya Wilaya hiyo,sambama na kutoa fedha kiasi cha shilingi laki nne kwa mwezi kusaidia chakula kwa shule zilizoko katika kata ya mbuguni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad