HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 6, 2020

KAMISHNA WA UHIFADHI KUTOKA TAWA ATEMBELEA VITUO VYAKE KATIKA MKOA WA MWANZA

 


KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Afande Mabula Misungwi Nyanda amefanya ziara ya kikazi kwenye vituo vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo Jijini Mwanza na kufanya mazungumzo na watumishi wa kikosi dhidi ya ujangili na klabu ya Malihai. 

Akizungumza kwenye kikao hicho mnamo tarehe 05/09/2020 Afande Mabula alijikita katika nyanja kuu tano (5) ambazo ni Uadilifu kwa Jeshi Usu, Mfumo mpya wa malipo (MUSE), Ukusanyaji wa mapato Pamoja na Tunu za TAWA. 

Aidha katika swala zima la uadilifu ameendelea kuwasisitiza Watumishi kuwa waadilifu wawapo kazini, huku akikemea vikali vitendo vya rushwa na kubainisha kuwa rushwa ni chanzo cha mikosi na yeyote atakayebainika kushiriki kwa hakika atachukuliwa hatua.

Ameendelea kusema kuwa kwa sasa TAWA imebadilisha mfumo wa malipo na kuingia kwenye mfumo wa MUSE ambao umeleta baadhi ya changamoto zilizopelekea kucheleweshwa kwa malipo hivyo amewasihi watumishi kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hichi cha mpito.

Aidha, Afande Mabula ameendelea kusisitiza kuhusu uongezaji wa makusanyo na kuinua mapato ya Shirika Amesisitiza watumishi kuongeza juhudi za kuhifadhi wanyamapori kwani ndio chanzo kikuu cha mapato na kuvumbua vyanzo vipya vya mapato kwa kutumia rasilimali adimu zinazisimamiwa na Shirika hilo.

Hata hivyo, katika kuboresha utendaji kazi watumishi walishauri Menejimenti ya TAWA kufuatilia gharama za ukamataji wa wanyamapori kwani zimekuwa kikwazo kwa wadau wanaohitaji kuanzisha mashamba ya wanyamapori.

 vile amewafahamisha watumishi ya kuwa Sheria ya Jeshi Usu imepitishwa na kwa sasa taasisi zote za uhifadhi zipo ndani ya jeshi moja linalotambulika kwa jina la Tanzania Wildlife and Forest Service ambapo pia hakusita kuwakumbusha watumishi kuzielewa na kuzitekeleza Tunu za TAWA ambazo ni uadilifu, ushirikiano, uwajibikaji, weledi na ubunifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad