BENKI YA NMB YAFUNGUA TAWI MALINYI MKOANI MOROGORO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 27, 2020

BENKI YA NMB YAFUNGUA TAWI MALINYI MKOANI MOROGORO

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi – Mathayo Masele na Kaimu Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Salie Mlay wakipiga makofi baada ya kufunguliwa rasmi kwa tawi la Benki ya NMB Malinyi
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro – Mathayo  Masele akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya NMB Malinyi . Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mikopo waa NMB – Demetus Kaguna, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB –  Salie Mlay – Meneja wa  NMB Kanda ya Mashariki – Dismas Prosper na Meneja wa Tawi la Malinyi – Ipyana Mwakatobe.
…………………………………………………………..
Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB Malinyi’ katika wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa wanasafiri umbali wa kilomita 160 kwenda mji wa Ifakara Wilayani Kilombero kupata huduma za kibenki.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi – Mathayo Masele amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua tawi ambapo anaamini litachochea ukuaji   wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo pamoja na uchimbaji wa madini ya dhahabu ambayo yamegunduliwa hivi karibuni.

Masele alisema kuwa Benki hiyo licha ya  kukuza uchumi pia itawapunguzia gharama wafanyabishara, na Taasisi ambazo zilikuwa zikitumia gharama kubwa kwaajili ya kusafirisha fedha kwa usalama zaidi Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Salie Mlay, alisema moja ya kichocheo kikubwa cha kufungua tawi hilo ni kuwasaidia wakulima na wafugaji waweze kupata mikopo pamoja na elimu ya ushirika utakaowapa tija kwa kutumia mfuko wa NMB Foundation.

Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi vikiwemoa mabati, kofia, misumari na mbao kwaajili yakukamilisha uwezekaji vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Nawigo iliyopo Malinyi. Ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad