TCRA imesitisha leseni ya utoaji huduma za utangazaji wa kituo cha Clouds TV na Redio kwa siku saba - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 27, 2020

TCRA imesitisha leseni ya utoaji huduma za utangazaji wa kituo cha Clouds TV na Redio kwa siku saba

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesitisha leseni ya utoaji huduma za utangazaji wa kituo cha Clouds Televisheni na Redio kwa siku saba kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 3, mwaka huu.

Aidha TCRA imekitaka kituo hicho kuanzia muda wa agizo hilo mpaka mwisho wa siku ya leo kuahirisha matangazo yote na kutumia muda wote uliobakia wa siku ya leo kuomba radhi kwa umma wa Tanzania kwa kukiuka Kanuni za Utangazaji kupitia kipindi cha Clouds 360.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad