WAKAZI WA DAR WAASWA KUNYWA MAZIWA KWA WINGI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 8 December 2019

WAKAZI WA DAR WAASWA KUNYWA MAZIWA KWA WINGI

Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akitoa vyeti kwa wawakilishi wa vilau vya jogging leo wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwl Julius K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam waaswa kuwa ya mfano katika kuhakikisha wanakunywa maziwa mengi zaidi.

Ameyasema hayo, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva wakati akizungumza na wanamichezo mbalimbali katika maonesho ya nne ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Jk. Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

"Kila jumapili ya Mwisho wa mwezi itakuwa siku ya kunywa maziwa tunaanza kwa mfano katika jiji la Dar es Salaam kwa kunywa maziwa kwa kila jumapili ya mwisho wa mwezi katika viwanja vya Sabasaba". Amesema Lyaniva.

Amesema kuwa maziwa ni mhimu na ni chanzo mhimu katika kuongeza kipato, pia ukinywa maziwa unakuwa na afya njema.

Lyaniva amesema zao pekee linaloweza kuvunwa kwa mwaka mzima ni maziwa ambayo unaweza kuvunwa kwa kila siku iendayo kwa Mungu ukilinganisha na mazao mengine yote.

"Katika mnyororo wa dhamani ya maziwa unazalisha fedha nyingi, na unapokuwa unafunga ng'ombe wa Maziwa unazalisha ajira kwa watu watakao kata majani, watu watakao kamua maziwa na watu watakao tembeza maziwa".

Hata hivyo Lyaniva amesisitiza ubora wa maziwa  kwa wadau wanaotengeneza na kuzalisha maziwa watengeneze yenye ubora wa hali ya juu kwani ubora ni mhimu sana katika afya.

Lyaniva ametoa wito kwa wananchi kuanza kufunga ng'ombe kwa wingi, ili tuweze kunywa maziwa kwa wingi kwa kuwa maziwa yanawingi wa virutubisho vingi. 

"Watu wanaokunywa maziwa wanakuwa na afya na furaha wakati wote na tuachane na kunywa maalikasusu mengine.

Aidha Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote amesema Bodi ya Maziwa inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka hadi kufikia lita 200 kwa mtu kwa mwaka.

Dkt. Sophia amewapongeza wadau wote walioshiriki katika kutoa hamasa kwa wananchi kuweza kunywa maziwa hasa baada ya mazoezi kwani maziwa yana virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ili kujenga afya.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maonesho ya viwanda ni tucheze tufanye mazoezi, tunywe maziwa kwa afya zetu.

Makampuni mbalimbali ya maziwa kama vile Dar fresh,Tangafresh, Asas Dairies, Woodland n.k walijitokeza kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wananchi kuweza kunywa maziwa mara baada ya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere (sabasaba).
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote akizungumza na vijana wa mbio ndogondogo wa wilaya za jiji la Dar es Salaam leo baada ya kutembelea katika viwanja vya maonesho ya JK. Nyerer Sabasaba jijini Dar es Salaam. Amesema Bodi ya Maziwa inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka hadi kufikia lita 200 kwa mtu kwa mwaka.

Baadhi ya wanajogging wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika katika viwanya vya JK. Nyerere Sabasaba katika Maonesho ya viwanda ya nne.Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akitoa vyeti kwa wawakilishi wa vilau vya jogging leo wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwl Julius K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akitembelea mabanda ya  kuuza maziwa leo wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwl Julius K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad