DK. MUSHI AOKOA ZAIDI YA WATOTO 400, NJITI NA WANAOZALIWA WAKIWA WAMECHOKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 8 December 2019

DK. MUSHI AOKOA ZAIDI YA WATOTO 400, NJITI NA WANAOZALIWA WAKIWA WAMECHOKA


Mbunifu Daktari Emmanuel Mushi akizungumza na wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia kwaajili ya kupata maelezo juu ya uunifu wa kifaa cha kuhifadhi joto la mtoto baada ya kuzaliwa.
Mfano wa mtoto akiwa katika kifaa cha kumuongezea mtoto joto baada ya kuzaliwa .MAZAO ya Tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH) yaonekana baada ya Mbunifu Daktari Emmanuel Mushi kuokoa watoto 400 ambao wamezaliwa wakiwa wamechoka na watoto njiti kwa kutengeneza mashine ya kuwaongezea joto (Incubator ya kuhifadhi joto la mtoto) katika hospitali ya Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mbunifu wa kifaa hicho Daktari Emmanuel Mushi amesema kuwa kifaa hicho kwa hapa nchini kinauzwa kwa bei rahisi zaidi ukitofautisha na vifaa ninavyouzwa nje ya nchi ikiwa vifaa hivyo vinafanya kazi ya aina moja.

Hata hivyo Dk. Mushi ameshauri Wizara ya Afya kumtumia kwa ufasaha katika kuzalisha mashine nyingi zaidi na kuzisambaza katika vituo vya afya ambayo hutoa huduma ya mama na mam na mtoto kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi ili kujenga taifa lenye watoto wengi na uchumi imara.

Mashine hizo ambazo zimetengenezwa kwa mfumo wa vifaa vya plastiki na kuunganishwa na umeme endapo joto la kifaa hicho litakuwa limepungua.

Dk. Mushi amesema katika kutengeneza mashine hiyo ya kuwaongezea watoto joto ambayo ameibuni mwenyewe amesema katika kufanikisha hilo ameshasaidia kujengwa kwa kituo cha afya ya mama na mtoto kilichopo katika mkoa wa Manyara ambapo wanawake wengi hufika na kujifungua katika kituo hicho.

Ameelezea kuwa kama mtoto njiti na ambaye amezaliwa akiwa amechoka joto lao hupungua kwa haraka baada ya kuzaliwa na kusababisha damu kuganda na kufariki.

Hivyo katika kupunguza vifo vya watoto njiti amesema kuwa  kifaa cha kutunza joto la mtoto pia ameshakifanyia utafiti na kugundua kifaa hicho kinafanya kazi vizuri alicho kipa jina la embranes womb kipo kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto ambao wanasafirishwa kutoka hospitali ya kijiji hadi hospitali ya Mkoa ambacho kinafanya joto la mtoto liweze kuwepo na kufanya damu itembee kwa urahisi mwilini.

Pia Dk. Mushi amewakaribishakatika maoneshoya nne ya viwanda viongozi wa wizara ya afya katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia waende wajionee vifaa vya kuwaongezea joto watoto. 

"Wizara ya afya ninawakabirisha katika maonesho haya ili mje mjionee mashine pamoja na kifaa cha kumsafirishia mtoto (embranes womb) kutoka vituo vya afya vya vijijini hadi hospitali ya mkoa kwani kimeshaanza kufanya kazi.

Amesema vifaa hivyo vikisambazwa katika vituo vya afya vilivyopo vijijini vitaweza kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi. 

"Malengo yangu ni kuokoa mamilioni ya watoto kwa kutengeneza vifaa vya kuwaongezea joto watoto pamoja na vifaa vya kuhifadhi joto kwaajili ya kumsafirishia mtoto kutoka hospitali ya ya vijijini hadi hospitali ya Mkoa".Amesema

Hata hivyo amewaasa serikali kuwekeza katika vifaa hivyo ili waweze kutengeneza vifaa vingi zaidi kwajili ya kuokoa watoto wachanga wanaokosa joto baada ya kuzaliwa.

Mbunifu Daktari Emmanuel Mushi akizungumza na wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia kwaajili ya kupata maelezo juu ya uunifu wa kifaa cha kuhifadhi joto la mtoto baada ya kuzaliwa.
Kifaa cha kuhifadhi joto ili kiweze kumfikisha mtoto kutoka hospitali za vijijini hadi hospitali ya Mkoa akiwa na joto linalotakiwa kwa afya ya mtoto.
Mtoto akiwa ndani ya kifaa  cha kuhifadhi joto na kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad