Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa -Mkuu wa Wilaya Mmanda. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 11 December 2019

Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa -Mkuu wa Wilaya Mmanda.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mtwara

 Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa kwani vitambulisho vya Taifa vinavyotumika katika usajili wa laini hizo ndio baadae watanzania tutatumbuliwa kwa kuwa na vitambulisho vya mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya uu Mtwara Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa Uhamasishaji wa Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Mmanda amesema changamoto kwa baadhi ya Wananchi wa Mtwara kupata vitambulisho ni kutokana na wanatoka nchi jirani ya Msumbiji hivyo lazima wafuate taratibu za Uhamiaji.

Amesema kuwa kila mtu ahakikishe anapata kitambulisho cha taifa ili aweze kusajili laini yake kwa alama za vidole kwani namba zitafungwa Desemba 31 na ambao hawatafanya namba hizo zisizosajiliwa zitafungwa na kugaiwa kwa watu wengine.

Amesema kuwa taarifa zilizosambaa katika mtandao ya kijamii kuwa zoezi la kuzima laini simu Desemba 31 kuwa limeongezwa ni kuzipuuza na kwamba zoezi liko palepale.

Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki Wananchi waache kununua simu Mkononi kwani kuna watu wanaweza kufanya uhalifu na mwisho wa siku mtu akaingia katika matatizo.

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko Amesema zoezi la usajili kwa Mkoa wa Mtwara lipo kwa Wilaya zote na kutaka Wananchi wajitokeze kupata kusajili laini za simu .

Amesema zoezi la kuzima simu liko palepale hivyo watu waache kupotosha zoezi hilo.Eseko Amesema kanda ya Mashariki wamezindua Uhamasishaji kumekuwa na matokeo makubwa kwa Wananchi kuhamasika katika kujisajili.

Afisa Usajili wa Mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Gide Magila amesema changamoto wanayokutana nayo ni watu kusajili majina mara Mbili na wakati mwingine kusahau kumbukumbu walivyosajili.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa alama  vidole katika uwanja wa Sabasaba mjini Mtwara. 

 Wananchi wakiwa katika foleni ya kuangalia namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa NIDA
 Afisa Msajili wa Mkoa wa Mtwara  wa Mamlaka ya a Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Gide Magila  akitoa changamoto wanazokutana na Wananchi wakati usajili na uangaliaji majina katika mfumo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akizungumza na Wananchi wakati wa Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mkoa wa Mtwara.
 Foleni ya Wananchi wakiwa katika ufatliaji wa namba za vitambulisho vya Taifa.

 Mabanda ya watoa huduma za simu kwa ajili ya kusajili laini za simu za  Wananchi kwa alama za vidole.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza namna kanda ya TCRA inavyohamasisha Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad