Benki ya CRDB na TTCL zaungana kuwasogezea Watanzania huduma za kifedha - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 10 December 2019

Benki ya CRDB na TTCL zaungana kuwasogezea Watanzania huduma za kifedha

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kulia) akibadilishana nyaraka na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude, baada ya kuingia makubalianao ya mpango wa pamoja wa kutoa huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi, katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji - TTCL, Mruta Hamis. Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akishuhudia uzinduzi wa huduma ya kuhamisha fedha kati ya SimBanking na T-Pesa uliofanywa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati akiongoza hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na wa TTCL wakifatilia hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 


Benki ya CRDB na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo wamezindua mpango wa pamoja kupitia huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema mpango huo unalenga katika kuwarahisishia wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti za CRDB kwenda T-Pesa, kuhamisha fedha kutoka T-Pesa kwenda akaunti yoyote ya CRDB pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia Simbanking.

“Lengo letu ni kuwapa wateja wetu uzoefu bora zaidi pindi watumiapo huduma ya SimBanking. Tunataka kuona mteja akiingia kwenye SimBanking USSD kwa kupiga *150*03# au SimBanking App aweze kumaliza mahitaji yake yote ya kifedha ‘One Stop Shop’ ikiwamo miamala ya T-Pesa,” alisema Raballa.

Raballa alisema ushirikiano huo na TTCL utataidia kusogeza huduma kwa watanzania wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini. Takwimu zinaonyesha ni asilimia 60 ya watanzania ndio wameunganishwa na mfumo wa kifedha kupitia simu za mkononi, wakati ni asilimia 17 tu ya watanzania ndio wanaotumia huduma za kibenki.
“Benki ya CRDB inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma za kifedha, hatua ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wetu wa taifa letu. Tunafurahi kushirikiana na TTCL katika kufanikisha azma hii "aliongezea Raballa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa T-Pesa, Lulu Mkude, alisema ushirikiano huo ni mafanikio makubwa kwa TTCL, kwani utawawezesha maelfu ya watanzania wote wa mijini na vijijini kupata huduma za kifedha za kwa urahisi.

Lulu alisema TTCL kuunganishwa kwa huduma ya T-Pesa na SimBanking kutawasiaidia wateja wa Benki ya CRDB kuweka pesa kwa urahisi kwenye akaunti zao kupitia T-Pesa lakini pia kuongeza salio au kuwatumia ndugu jamaa na marafiki fedha kwenye akaunti zao za T-Pesa.

''Kufurahia huduma mteja atatakiwa kuingia katika menu ya T-Pesa kwa kupiga *150*71#, na kisha kuchagua huduma ya SimBanking,” alisema Lulu Mkude, huku akisisitiza kwamba hivi sasa TTCL imejipanga vilivyo kusogeza mawakala wake wa T-Pesa karibu zaidi na wananchi hususani vijijini ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad