TCRA yapeleka kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako mkoa Mtwara - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 11 December 2019

TCRA yapeleka kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako mkoa Mtwara


 
 
 
Mtwara Jumatano 11 Disemba 2019

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeini ya ‘Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha Usajili mkoani Mtwara huku ikiwahimiza mwananchi wa mkoa kukamilisha usajili wa laini zao za simu kwa alama ya vidole kabla ya mwisho wa mwezi.

Kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha usajili ya laini ni ushirikiano wa makampuni yote ya simu za mkononi hapa nchini huku ikisimamiwa na TCRA kwa udhamini wa FSDT.

Akizungumza Mtwara wakati wa kuzindua kampeini hiyo ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako, Mmwakilishi wa TCRA Kanda ya Mashariki Viollet Essoko amesema changamoto zilizopo zimekuwa zikifanyiwa kazi na kusisitiza kuwa licha ya kuwekwa matangazo ya kuhamasisha umma haachwi mtu nyuma kamilisha usajili bado kuna wananchi wanasua sua kufuatilia michakato ya NIDA ili kupata namba na kusajili line zao za simu.

Amesema idadi kubwa ya vijana wamekuwa wakipuuzia zoezi hilo huku watu wenye umri mkubwa wameonyesha kujitokeza kwa wingi kufuatilia vitambulisho vya nida lakini pia kusajili line zao za simu.

Wakati huo huo, baadhi ya wakazi wa mkoa wa mtwara ambao bado hawajapatiwa vitambulisho vya taifa vya NIDA wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji na vitendea kazi ili kurahisisha zoezi hilo ambalo kwa sasa limekuwa na muamko mkubwa kwa wakazi wake.

Wakazi hao wametoa ombi hilo kutokana na kukaa kwenye foleni ili kupata huduma hiyo kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo ipasavyo.

Hata hivyo wakazi hao wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji sambamba na vitendea kazi ili zoezi hilo liweze kwenda kwa haraka hasa kipindi hiki ambacho idadi ya watu imeongezeka.

Mapema akifungua zoezi hilo ambalo litadumu takribani wiki nzima katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda amewataka wananchi kutopuuzia zoezi hilo ambalo umuhimu wake ni mkubwa.

Amesema huwezi kuitwa Mtanzania kama huna kitambulisho cha NIDA na kuwataka watambue kuwa huduma muhimu zitapatikana tu kwa mtu mwenye kitambulisho cha nida na hivyo kuwasihi kukamilisha zoezi la nida na kupata usajili wa laini zao za simu.

Zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatarajiwa kukamilika disemba 31 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad