HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 12, 2019

HOSPITALI YA TEMEKE YAPOKEA MASHINE MBILI ZA PATIENT MONITOR SYSTEM KUTOKA SWISSPORT

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Hospitali ya Temeke wamepokea mashine mbili za Patient Monitor System zenye thamani ya Milioni 12.6 kutoka kwa kampuni ya Swissport Tanzania.

Mashine hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Mrisho Yassin kwa Kaimu Mganga Mkuu Wa Hospitali ya Temeke Dkt  Serafini Patrice.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Yassin amesema wameweka malengo ya kusaidia jamii na wameanza na hospitali ya Temeke kwa kuwaletea mashine hizi mbili zitakazowasaidia kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wenye uhitaji.

Yassin amesema, wanatambua Wanatoa huduma kwa wagonjwa wengi sana ila wameanza kutoa mashine mbili ambazo zitaenda kwa watoto na wakina mama na kila mashine ikiwa na gharama ya Milioni 6.3.

" Tunafahamu uhitaji wa wagonjwa, inasaidia kupima mfumo mzima wa afya ya binadamu ila sisi tungependelea moja iende kwa watoto na nyingine kwa wakina mama,"amesema.

"Hospitali hii inahudumia wagonjwa Milioni 1.6 kwa mwaka, na Swissport wafanyakazi wake wengine wanaishi Temeke tunaamini wanatibiwa hapa kwahiyo tuliamua kuanzia hapa," 

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dkt Patrice amewashukuru kampuni ya Swissport kwa kuona umuhimu wa kuleta mashine hizo zenye uhitaji mkubwa sana kwa wagonjwa.

Dkt Patrice amesema, uongozi wa Swissport uendelee kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kuendesha hospitali hizi kwa kutoa misaada mbalimbali.

"Tunaona serikali ya awamu ya tano inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha inawekeza zaidi katika afya na kuwaomba wadau wengine waendelee kutoa msaada huo kwani bado wana uhitaji wa mashine hizo,"

Dkt Patrice  ameeleza kuwa mashine zilizoletwa na Swissport zitasaidia sana kwani wamekuwa wanakosa kuwahudumia wagonjwa na kuwahamishia Muhimbili ila baada ya kufika kwa mashine hii zitasaidia sana.

Kampuni ya Swissport inashughulika na kuhudumia mashirika ya ndege,abiria, mizigo na Viwanja vya ndege na kwa Tanzania wanatoa huduma kwenye Viwanja cya ndege vya Dar es Salaam,, Kilimanjaro, Songwe na Mtwara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swissport Mrisho Yassin akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu Wa Hospitali ya Temeke Dkt  Serafini Patrice mashine mbili za Patient Monitor System zenye thamani ya Milioni 12.6 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wenye uhitaji hususani watoto na wakina mama
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swissport Mrisho Yassin akizungumza na waalikwa waliofika wakati wa ukabidhiji wa mashine mbili za Patient Monitor System zenye thamani ya Milioni 12.6 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wenye uhitaji hususani watoto na wakina mama
Kaimu Mganga Mkuu Wa Hospitali ya Temeke Dkt  Serafini Patrice mashine mbili za Patient Monitor System zenye thamani ya Milioni 12.6 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wenye uhitaji hususani watoto na wakina mama

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad