NSSF YAINGIA MAKUBALIANO YA KUPANGISHA NYUMBA NYUMBA ZAKE ZA MTONI KIJICHI KWA VYUO VITANO VYA ELIMU YA JUU JIJINI DAR ES SALAAM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 30 December 2019

NSSF YAINGIA MAKUBALIANO YA KUPANGISHA NYUMBA NYUMBA ZAKE ZA MTONI KIJICHI KWA VYUO VITANO VYA ELIMU YA JUU JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio (kulia) akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo jijini Dar es salaam wakati walipofika kukagua nyumba za NSSF za Mtoni Kijichi, kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kutumiwa kwa nyumba hizo na Wanafunzi wa Vyuo hivyo. Jumla ya Vyuo vitano vya Elimu ya Juu vimeonyesha nia ya kuchukua nyumba hizo kwa ajili ya makazi ya Wanafunzi wake. Vyuo hivyo ni Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo cha Usimamizi Fedha (IFM), Chuo cha Uhasibu (TIA) pamoja na Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi Dar es salaam (DIT).

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kusaini mikataba wa makubaliano ya kutumiwa kwa nyumba za NSSF za Mtoni Kijichi na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu zaidi ya vitano, vya jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Maluka wakisaini Mkataba wa Makubaliako ya kutumiwa kwa nyumba za NSSF za Mtoni Kijichi na Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali vya jijini Dar es salaam, katika hafla fupi iliyofanyika leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio akipeana mkono na Naibu Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Usimamizi Fedha (IFM), Imanuel Mnzava  baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliako ya kutumiwa kwa nyumba za NSSF za Mtoni Kijichi na Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali vya jijini Dar es salaam, katika hafla fupi iliyofanyika leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio pamoja na Makamu Mkuu wa Utawala na Fedha wa Chuo cha Teknolojia ya Ufundi Dar es salaam (DIT), Dkt. Najat Mohamed wakisaini Mkataba wa Makubaliako ya kutumiwa kwa nyumba za NSSF za Mtoni Kijichi na Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali vya jijini Dar es salaam, katika hafla fupi iliyofanyika leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad