KANISA LA MRM-BIF LATOA ZAWADI KWA WATU WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KEREGE BAGAMOYO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 31 December 2019

KANISA LA MRM-BIF LATOA ZAWADI KWA WATU WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KEREGE BAGAMOYO

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF)  Moses Emena akikabidhi zawadi kwa ajili ya Sikukuu kwa mzee asiyejiweza baada ya kuwatembelea katika Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo.

Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF) limetoa zawadi ya chakula kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu katika Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo wa Chakula, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Moses Emena amesema wametoa zawadi hizo kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu ili na wao washerehekee sikukuu kama watu wengine  katika jamii zao ili kuwapa thamani kubwa.

Mchungaji Emena amesema, watu waliowagusa katika zawadi hizo ni wajane, yatima, walemavu na wale wasiojiweza lengo likiwa ni kuonesha upendo wa Kristo kwa watu wote na kutambua umuhimu wa kila mtu katika jamii na  kuwapa furaha.

Amesema, zawadi hizi zimeenda kwa watu 50 walionufaika na kuwakabidhi mchele, sukari na sabuni ambapo watafurahi na kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya kwa kuondoa unyonge na kuwarudishia furaha ndani ya mioyo yao.

"Tukio hili limeleta mwako   na hamasa chanya kwa watu hawa wanaoishi katika mazingira kwenye Wilaya ya Bagamoyo na kutambua umuhimu wa kila mtu na kuondoa matabaka waliyojijengea na kuhimiza upendo,"amesema

Aidha, Emena amewashukuru wadau wote waliokubali kujumuika na kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye tukio hilo, pia waumini wa kanisa la MRM-BIF Kerege Kitonva kwa  maandalizi mazuri.

Pia, amewashukuru wadau wa maendeleo kwa ufadhili waliouonesha katika kuelekea tukio hilo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF)  Moses Emena akikabidhi zawadi ya sikukuu kwa  wanafunzi wanaoishi maizngira magumu baada ya kuwatembelea katika Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF)  Moses Emenaakikabidhi zawadi kwa ajili ya Sikukuu kwa mzee asiyejiweza baada ya kuwatembelea katika Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF)  Moses Emena akikabidhi zawadi ya Sikukuu kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, yatima, wajane na wasiojiweza.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mighty Revival Ministries Berea International Fellowship (MRM-BIF)  Moses Emena akiwa katika picha ya pamoja baada ua kukabidhi zawadi ya Sikukuu kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, yatima, wajane na wasiojiweza.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad