NI AZAM DHIDI YA BIASHARA UNITED SIKU YA IJUMAA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 November 2019

NI AZAM DHIDI YA BIASHARA UNITED SIKU YA IJUMAA

N a Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TIMU ya Azam Fc imeendelea na mazoezi yake kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Biashara United utakaochewa siku ya Ijumaa Uwanja wa Chamazi Complex.

Mchezo huo wa raundi ya nane ya Ligi kuu utapigwa kuanzia majira ya saa 1 huku Azam, ukiwa ni mchezo wa pili mfululizo uwanja wa nyumbanu.

Wachezaji wa Azam wameendelea na mazoezi yao,chini ya Kocha Aristica Cioaba aliyeanza kibarua chakemcha kuinoa timu hiyo wiki ya pili sasa.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera, Azam ilishindwa kuibuka na ushindi na kuambulia suluhu ya kutokufungana mpaka dakika 90 zinamalizika.

Azam ipo katika nafasi ya 14 wakiwa na alama 10 wakicheza michezo sita na Biashara ikiwa nafasi ya 16 na alama zake 08 akiwa na michezo tisa.
Wachezaji wa Azam wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United siku ya Ijumaa saa 1 jioni Chamazi Complex.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad