NAIBU WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI BASEKI KWA KUIHUJUMU SERIKALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 2 November 2019

NAIBU WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI BASEKI KWA KUIHUJUMU SERIKALI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Mhandisi Leonard Baseki kwa kuihujumu serikali na kushindwa kukamilisha mradi wa maji Mkuranga.

Akizungumza baada ya kupata taarifa ya mradi wa maji Mkuranga, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara kufuatilia suala hilo na kumsimamisha kazi mhandisi huyo kwa kuihujumu serikali.

Aweso amesema, mhandisi wa maji Baseka ameshindwa kutekeleza mradi huo na kuishia kuihujumu serikali zaidi ya Bilion 2 kwa kujenga mradi ambai hauna chanzo cha maji.

" Haiwezekani mhandisi tena wa serikali anaharibu hapa Mkuranga halafu anahamishiwa sehemu nyingine na kule anaenda Kuharibu pia kwahiyo nimemuagiza Katibu Mkuu amsimamishe kazi na apelekwe kwenye bodi ya wahandisi," amesema.

Aweso amesema, tayari wahandisi 95 wameshaondolewa kutokana na kutokukamilisha miradi na kuiingiza serikali  hasara na kuchelewesha adhma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani

"Nawaonya wahandisi wengine kuwa hatutafumbia.macho pindi wanapohujumu Serikali tutawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka mbele ya kamati ya maadili," amesema

Akizungumzia mradi wa maji wa Mkuranga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA, Aweso amemtaka Mkandarasi wa mradi huu kwenda kwa haraka ili wananchi wapate maji kwa wakati kama makubaliano yalivyo kwenye mkataba.

Zaidi, Aweso amesema amewaagiza  DAWASA kufanya kikao cha pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Mkuranga na kufanya usanifu wa mradi wa Maji ili wakazi wote wa Mkuranga wapate maji.

"Nawapongeza DAWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendesha miradi, kwa fedha zao za ndani hili ni jambo kubwa sana tumeona Dar es Salaam wamefanya kazi na sasa wameamua kuja Mkuranga ili wananchi mpate maji safi na salama," amesem Aweso.

Aweso ameendelea na ziara yake ndani ya Mkoa wa Pwani wa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuweza kumtua mama ndoo kichwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Mhandisi Bakari Mgaya wakati alipotembelea miradi ya maji Mkuranga Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Bakari Mgaya alipofika kulikagua tanki la maji lililopo kwenye hatua ya uienzi litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion 1.5 na kuhuhudumia wakazi 25,000 kwa siku Mkuranga Mkoani Pwani
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisalimiana na Katibu wa Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, Omar Kisatu baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkuranga leo.
Vifaa na mabomba yanayotumika kulaza kwa ajili ya usambazaji wa maji Mradi wa Mkuranga.
Msimamizi wa  Mradi wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA  Mhandisi Bakari Mgaya akisoma taarifa ya mradi ws Mkuranga ambao umefikia hatua ya ujenzi wa tanki la Lita Milion 1.5 wenye thamani ya Bilion 5.5 wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso leo Mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati alipotembelea miradi ya maji ya Wilaya hiyo leo Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na watendaji mbalimbali wa Mamlaka za Maji, watendaji wa serikali wakati alipotembelea miradi ya maji Mkuranga leo Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiyaonja maji yanayotoka katika chanzo cha maji asilia kitakachopeleka maji kwenye tanki linalohifadhi maji Lita Milion 1.5 lililopo kwenye hatua ya ujenzi litakalohudumia wakazi 25,000.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad