MKWASA AWATAKA WACHEZAJI WA YANGA KUJITUMA, NI WACHEZAJI WAZURI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 6, 2019

MKWASA AWATAKA WACHEZAJI WA YANGA KUJITUMA, NI WACHEZAJI WAZURI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha Yanga cha wachezaji 20 kimeondoka leo kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda utakaohezwa siku ya Ijumaa.

Mchezo huo wa raundi ya nane, na Yanga ukiwa mchezo wake wa tano wakiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa aliyechukua mikoba ya Kocha Zahera Mwinyi, Mkwasa atasaidiwa na Said Maulid, Meneja na Mratibu wa timu akiwa Dismas Ten, Kocha wa Magolikipa ni Peter Manyika.Kocha Mkwasa amezungumza na wachezaji baada ya kukutana nao kuwataka kuhakikisha wanapambana na kupata matokeo na lengo la kwanza la kila mchezaji anaekuja hapa ni kuhakikisha Yanga inabeba ubingwa .

"Ni lazima tuanze kushinda mechi zetu. Hamtachukiwa na mashabiki kama mtacheza vizuri na kushinda. Maisha yenu yatakua mazuri sana. Watu watakuja viwanjani na mtalipwa kwa wakati .Nyie ni wachezaji wazuri sana na mimi niko hapa kuwasaidia kulifanikisha hilo." amesema 

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kikosi cha wachezaji 20 kimeondoka leo na tayari wameshawasili mkoani Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Ndanda siku ya Ijumaa.

Amesema, Wachezaji kadhaa wamebaki jijini Dar es Salaam,wachezaji hao ambao hawajasafiri na timu ni Paul Godfrey, Mohamed Issa, Maybin Kalengo, Abdul Aziz Makame ambao wote ni majeruhi huku Feisal Salum akiwa na matatizo ya kifamilia. 

Mkwasa aliwahi kuifundisha Yanga katika msimu tofauti akiwa chini ya Kocha Mkuu Hans Van Pluijm, na walipata mafanikio makubwa katika kikosi hicho ikiwemo kuipa ubingwa Yanga na kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wana pointi saba nafasi ya 18 imecheza mechi nne pekee huku wapinzani wao Ndanda imecheza jumla ya mechi 8 imejikusanyia pointi saba zinazoifanya iwe nafasi ya 19 .
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad