MMILIKI WA KISIMA ASIPOJISAJILI HATATOA HUDUMA YA MAJISAFI KWA WANANCHI-DAWASA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 October 2019

MMILIKI WA KISIMA ASIPOJISAJILI HATATOA HUDUMA YA MAJISAFI KWA WANANCHI-DAWASA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewataka wauzaji wa majisafi kwa kutumia visima binafsi wafike katika ofisi za Mamlaka hiyo kuanzia Oktoba 28 kwa ajili ya kuwatambua na kuwasajili kama watoa huduma Mbadala wa Dawasa kwenye maeneo yao.

DAWASA imewataka wamiliki hao waliopo ndani ya Dar es Salaam kufika na taarifa za wateja wanaowahudumia, vyeti vya ubora wa maji na taarifa za visima.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mamlaka hiyo, ikiwataka watoa huduma kufika ofisi za Dawasa Gerezani.

Dawasa imeendelea kusisitiza kuwa dhumuni la zoezi hilo ni utambuzi wa watoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za majisafi kwa wananchi.

Aidha, Mamlaka ya Dawasa ndio chombo kilichokasimiwa kisheria kusimamia huduma za usambazaki maji safi ndani ya eneo lake la huduma ambalo ni jijji la Dar es Salaam, Miji ya Mlandizi, Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Ili kutimiza matakwa ya kisheria, Dawasa imeanza kuwatambua na kuwasajili kwa kuwapatia cheti cha utoaji huduma za maji safi kwa watoa huduma za maji

Na ikumbukwe kuwa, zoezi hili la utoaji vyeti litafanyika kwa muda wa mwezi mmoja baada ya tangazo hili na muda wa usajili ukipita mtoa huduma yoyote asiye na cheti cha kutoa huduma hataruhusiwa kuuza maji.

Mamlaka imeweka wazi kuwa hakutakuwa na tozo yoyote katika zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad