MAONESHO YA SITE YAZIDI KUTANUA WIGO WA BIDHAA ZA UTALII KUTOKA TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 20 October 2019

MAONESHO YA SITE YAZIDI KUTANUA WIGO WA BIDHAA ZA UTALII KUTOKA TANZANIA

Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

WAFANYABIASHARA wadogo wa bidhaa za utalii wamefanikiwa kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa kwa kutumua mfumo wa Speed Networking .

Hayo yamefanyika kwenye maonesho ya Utalii yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Saalam.

Bodi ya Utalii Nchini (TTB) wameendelea kuandaa Maonesho ya Swahili International Tourism Expo (SiTE) 2019 kwa mara ya tano na jumla ya kampuni za waoneshaji 210 kutoka nchi 60, Jumla ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari takribani 333.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Mratibu wa Maonesho ya SiTE ambaye pia Meneja Huduma za Utalii Joseph Sendwa amesema onesho hili linawafaidisha mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.

Amesema, bodi ya utalii imekuwa inaenda sokoni kutaganza utalii na kuweza kuandaa maonesho ili kuwakutanisha wadau wa utalii kutoka pande zote duniani.

Pia, Sendwa amesema wafanyabishara wa utalii wameweza kuunganishwa na wadau wakubwa wa utalii na kufanya appointment moja kwa moja kwa kutumia  mfumo wa Speed Network ambao ni rahisi sana.

"Wafanyabiashara wa bidhaa za utalii wameweza kufanya mazungumzo na wadau wakubwa na kuweka makubaliano na hii imewasaidia kupata mazungumzo nao ya kibiashara na wanunuaji tofauti," amesema

Sendwa ametoa wito kaa watanzania hususani mawakala wa masuala ya utalii wakubwa na wadogo kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho ya SITE kujionea bidhaa mbalimbali.

Aidha, TTB imeandaa ziara kwa ajili ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari wa kimataifa Oktoba 21, kwenda kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya asili ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Maeneo mengine ni Fukwe za Tanga na mapango ya Amboni, Misitu ya Magoroto, Mlima Kilimanjaro na miradi ya utalii wa utamaduni katika Mkoa wa Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Riaha na Mji wa Iringa. Pia Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa na Mikumi, Visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Pia, katika maonesho hayo kumekuwa na semina  zinazoendeshwa  na wataalamu waliobobea kwenye masuala ya utalii kukiwa na mada mbalimbali.
Mratibu wa Maonesho ya SiTE ambaye pia Meneja Huduma za Utalii Joseph Sendwa akizungumzia maonesho ya utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE) 2019 yanavyozidi kukua na kuvutia wadau wa utalii na fursa wanazozipata mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.
linawafaidisha mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad