HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 20, 2019

MFAHAMU MWANA HABARI ALIYEJIKITA KATIKA MASUALA YA UTALII

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Maonesho ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SiTE) yameweza kuwavutia hususani wajasiriamali wadogo wanaozalisha mazao ya utalii nchini.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Mjasiriamali mdogo ambaye pia ni muanzilishi wa Asili Style, Glory Meiseyeki amesema kuwa hii ni mara yao ya kwanA kushiriki katika maonesho hayo ya (SiTE)  na wameweza kukutana na wadau mbalimbali.

Amesema, wazo la kuanzisha kutengeneza bidhaa za utalii ni baada ya kupata wazo hilo wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya TBC Safari alipowavalisha baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho.

Glory amesema, maonesho ya mwaka huu ni mazuri na yeye ni mara yake ya kwanza kushiriki ila ameona fursa nyingi ikiwemo kuzungumza na wadau mbalimbali wa bidhaa za utalii 'Speed networking'.

"Unakutana na watoa huduma tofauti, kutoka nchini tofauti mnakutana na kufanya mazungumzo pamoja na kubadilishana mawasiliano,"amesema Glory.

"Asili style imeanzishwa mwaka huu, na imejikita katika kuzalisha na uuzaji wa bidhaa za utamaduni ambapo tumeanzia nguo za kimasai ambapo zina rangi nyingi unaziweza kuzielezea, utungaji wa shanga na vingine zaidi,"

Glory ni mwaandishi wa habari aliye mbunifu na kupenda masuala ya utalii na kuamua kujikita zaidi katika kuwa mbunifu wa mitindo mbalimbali ya kitalii kwa kutumia nguo na bidhaa za Kimasai.
Mwanahabari Glory Glory Meiseyeki, mjasiriamali mdogo na Mwanzilishi wa Asili Style akionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza kwa kutumia utamaduni wa asili ya Kimasai katika maonesho ya tano ya Utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE)  2019.
Mwanahabari Glory Glory Meiseyeki, mjasiriamali mdogo na Mwanzilishi wa Asili Style akitoa maelezo mbalimbali kwa wateja waliofika kutembelea band lake ndani ya maonesho ya ya tano ya Utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE)  2019



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad