BENKI YA CRDB YADHAMINI MAONYESHO YA UTALII YA SITE JIJINI DAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 19 October 2019

BENKI YA CRDB YADHAMINI MAONYESHO YA UTALII YA SITE JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati akiwasilisha mada katika warsha iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Benki ya CRDB ambao ni miongozi mwa wadhamini wa maonesho hayo, imeelezea fursa mbalimbali inazozitowa kwa wateja wakena namna inavyoweza kubadilisha sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akifafanua jambo katika warsha iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu akielezea jambo juu ya mikopo ya magari ya Utalii kwa baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Automechs Limited ( HAL), Satbir Hanspaul ambaye pia ni mbia wa Benki ya CRDB anayetengeneza na kuuza magari maalumu ya Utalii nchini, akifafanua jambo juu ya namna magari hayo yanavyoweza kuwa katika warsha hiyo, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad