DAWASA YAKESHA USIKU NA MCHANA KUREJESHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA KEREGE, AMANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 22 October 2019

DAWASA YAKESHA USIKU NA MCHANA KUREJESHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA KEREGE, AMANI

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imejikuta ikikekesha usiku na mchana katika kuhakikisha inarejesha maji kwa wakazi wa maeneo ya Kerege hadi Amani, Bagamoyo kufuatia kukatika kwa bomba kuu la inchi 54 linalosafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Meneja usambazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Eng. Tyson Mkindi amesema kuwa maji yalikuwa yamekatika kwa siku tatu mfululizo.

"Jitihada za kuwarejeshea maji wakazi wa maeneo mbalimbali zipo katika hatua za mwisho ingawa  kazi ya kurekebisha bomba hilo imechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kuwepo kwa maji mengi katika mto Rufijii". Amesema Eng. Mkindi.

Eng. Mkindi amesema kuwa, chanzo cha kukatika kwa bomba hilo kuu na kushindwa kusafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini inasababishwa na uchimbaji holela wa mchanga katika mto Rufiji na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

Hata hivyo Dawasa imechukua hatua ya dharura kwa kuchepusha maji kutoka katika bomba jipya la inchi 72 na kuyaingiza katika bomba la zamani la zege ambalo litazibwa kabla na baada ya mto ili kuruhusu wananchi walio kosa maji kutoka maeneo hayo kupata huduma hiyo kama awali. Amesema Eng. Mkindi

Aidha maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa bomba hilo ni Kerege, Mapinga, Kiharaka, Kiembeni, Mingo, Kilemela, Kimele, Vikawe, na Amani.
 Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Said Leonard(kushoto) akitoa maelekezo kwa dereva wa Tingatiga lililokuwa linaweka bomba vizuri wakati wa matengenezo ya bomba  na kuchepusha maji kutoka katika bomba jipya la inchi 72 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo ili kuweza kupatikana kwa maji katika maeneo yalipokatika kwa muda. Wa kwanza kulia ni Kaimu Meneja usamabazaji maji wa Dawasa, Eng. Tyson Mkindi.
 Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam(DAWASA), Steven Kirigo akichomelea bomba la  inchi 72 ili kuchepusha maji kwa ajili ya upatikanaji wa maji haraka kwa wateja ili kuendelea kutengeneza bomba la zamani wakati wateja wanapata maji. 
  Kaimu Meneja usamabazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Eng. Tyson Mkindi akitoa maelekezo wa mafundi wa waliokuwa wanatengeneza bomba hilo katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo usiku wa kuamkia leo ili wananchi waweze kupata maji kwa haraka.
 Tingatinga likiweka Chuma kwenye maungio ya bomba ili kuweza kuunganishwa.
Picha na Michuzi Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad