CHAMA CHA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII CODEPATA CHAJIZIDHATITI KULETA MABADILIKO KATIKA JAMII - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 October 2019

CHAMA CHA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII CODEPATA CHAJIZIDHATITI KULETA MABADILIKO KATIKA JAMII

Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya jamii nchini CODEPATA kimejidhatiti katika kuhakikisha wanaifikia jamii na kuwpa elimu ya juu ya kujitegemea na kutumia fursa na rasirimali walizonazo kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Rais wa Chama cha Maendeleo ya Jamii CODEPATA Bw. Sunday Wambura katika siku ya tatu ya Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendelea jijini humo.

Bw. Wambura amesema kuwa Chama hicho kimejipanga katika kusimamia pia maadili ya Kada ya Maendeleo ya Jamii na kuepusha wavamizi wanajiita Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ili kuwa na Kada yenye misingi dhabiti katika kutekeleza majukuu yake.

“Kuna watu wengi hapa Nchini ambao walikuwa wanajiita wataalamu wa Sekta hii lakini kwasasa chama kitaweza kuwatambua wataalam sahihi kutokana na usajili lakini pia wataweka mwongozo utakaotumika katika utekelezaji wa majukumu ya wataalam wa maendeleo ya jamii.”Aliongeza Bw. Wambura.

Ameongeza kuwa mwongozo wa Taaluma hiyo uliotolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kuwa umetolewa kwa wakati kwani utakiwa nguzo muhimu kwa wataalam hao kuweka vizuri shughuli zao na kutambua vyema kazi na huduma zinazotolewa na wataalam wa Maendeleo ya Jamii.

Aidha Bw. Wambura amesema awali watu walidhani wataalam hao ni wa Serikali tu lakini sasa kuna wataalam wa Sekta hiyo wanaopatika na katika Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali na baadhi yao ni wanachama wa CODEPATA hivyo chama hicho kinafikiria pia kuanzisha mwongozo ambao utatumika kwa wanachama wote.

“Tutakitumia chama chetu katika kuhakikisha jamii ya kitanzania inabaili fikra na kujihusisha katika shughuli za maendeleo katika maeneno yao” alisema Bw. Wambura

Naye Mratibu wa Chama cha Maendeleo ya Jamii Kanda ya Mashariki Bw. Wanjoke Chinchibera amewataka vijana pamoja na wataalam wa taaluma ya Maendeleo ya Jamii walio nje ya chama kuendelea kujisajili ili waweze kufaidika na huduma za chama lakini pia kukipa nguvu chama hicho ili kiweze kutetea na kulinda maslahi ya taaluma yao.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mwanachama wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii CODEPATA Bi. Angela Mvaa amesema kuwa Chama hicho sio cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wenye ajira pekee bali kwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii walio katika ajira rasmi na walio nje ya ajiri na wale waliomaliza masomo ya Maendeleo ya jamii nchini.

Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad