SERIKALI KUSHUGHULIKIA USHURU WA ZAO LA GUNDI WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 6 September 2019

SERIKALI KUSHUGHULIKIA USHURU WA ZAO LA GUNDI WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu,akitoa maagizo juu ya uhumhimu wa kutunza mbuga ya Wembere pamoja na miti yake ya asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
Meneja Misitu Wilaya ya Iramba, Shaban Nyamasagara (wa kwanza kushoto) ,akitoa maeelezo juu ya utunzani wa miti aina ya migunga inayoongoza kwa kuzalisha gundi duniani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu (mwenye kombati). alipofanya ziara ya kukagua shamba la miti aina ya migunga wilani Iramba mkoani Singida hivi karibuni.
Wakala wa Kampuni ya Mohammed Enterpriseses Kija,akitoa maombi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza ushuru na tozo ili iweze kupata soko na kunufaisha wakulima,wafanyabiashara na serikali yenyewe.


Na Nathaniel Limu, Singida

SERIKALI imeahidi kuyafanyia kazi maombi ya mawakala na wanunuzi wa zao la gundi wilaya ya Iramba yanayohusu punguzo la ushuru unaotozwa kwa madai unachangia zao hilo likose wananunuzi.

Ahadi hiyo imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Costantine Kanyasu,muda mfupi baada ya kukagua shamba la miti aina ya migunga (vachellia drepanolobium) inayoaminika kuzalisha gundi nyingi zaidi duniani.

Alisema majukumu ya serikali ni pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili biashara zao ziwe na tija kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.“Maombi yenu nimeyapokea tutayafanyia kazi mapema iwezekanavyo na tukijiridhisa na hicho mnachokisema serikali yenu sikivu itafanya maamuzi ambayo yatazingatia pande zote za Serikali na wafanyabishara ili kunufaika na zao la gundi”, alisema.

Kanyasu alisema kuwa mbunga ya Wembere iliyopo katika mikoa ya Singida,Tabora,Shinyanga na Simiyu,itapandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya taifa hiyo italindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria.

“Nashukru kusikia uongozi wa vijiji vinavyoizunguka mbuga hii wameridhia iwe hifadhi na kwamba watailinda kwa nguvu zao zote miti hii ya asili migunga ili iendelee kunufaisha kizazi cha sasa na cha baadae ”,alisema.

Katika hatua nyingine Kanyasu aliagiza wavamizi wote waliovamia chanzo cha maji cha bwawa la Urughu watolewe haraka katika maeneo hayo ili kunusuru chanzo hicho kukauka.Kwa upande wake Meneja Misitu wa Wilaya ya Iramba, Shaban Nyamasagara, alisema mbunga ya Wembere ina umuhimu kulindwa na kutuzwa kwa kuwa ina uoto wa asili wa nyasi.

“Nyasi hizi zinasambaa sehemu kubwa ya mbunga na ni muhimu katika uwepo na uhai wa ziwa Kitangiri na Eyasi.Maziwa haya ni vyanzo vikubwa vya uchumi kwa jamii inayoyazunguka maziwa hayo”, alisema Nyamasagara.

Alitaja changamoto za hifadhi hiyo kuwa ni baadhi baadhi ya watu kuvamia mara kwa mara kwa shughuli za kibinadamu na uelewa duni wa wananchi kuhusu mambo ya uhifadhi wa taifa na kuwa eneo la Wembere kukosa miundo mbinu ya barabara za kupitika kipindi cha masika na kiangazi.

Mawakala na wanunuzi wa zao hilo walisema kuwa hivi sasa soko la dunia la gundi bei imeteremka hivyo kununua kwa sasa na kulipa ushuru na usafirishaji ni lazima mfanyabiashara atapata hasara na kufilisika.

Wakala wa Kampuni ya Mohammed Enterprises, Zengo Kija, alisema biashara ya gundi kwa sasa inasuasua na mambo yasiporekebishwa haraka mvua zikianza kunyesha shehena za zao hilo zilizopo kwenye maghala na kwa wananchi itaharibika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad