HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 6, 2019

MIRADI YA NISHATI YAJADILIWA KWENYE MKUTANO WA TUME YA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA UGANDA

Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, ulioanza Septemba 3 mwaka huu, umehitimishwa jana, Septemba 5 jijini Dar es Salaam; ambapo miradi ya nishati ni miongoni mwa iliyojadiliwa.

Akifunga mkutano huo, ngazi ya Mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, aliwaeleza wajumbe kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda umeendelea kuimarika siku hadi siku kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa katika sekta kadhaa, ambayo ni pamoja na nishati.

“Kwa sasa tunatekeleza miradi kadhaa ya ushirikiano, ukiwemo wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), mradi wa kuzalisha umeme wa maji (megawati 14) wa Kikagati – Murongo, mradi wa umeme wa maji Nsongezi na mingine mingi.”

Katika Mkutano huo wa siku tatu, pamoja na mambo mengine, ulipokea taarifa ya Wizara ya Nishati ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Mkutano wa Pili wa Tume husika, uliofanyika Agosti, mwaka jana, jijini Kampala, Uganda.

Mbali na miradi iliyotajwa awali; Taarifa hiyo ya Wizara ilijikita pia katika masuala ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika bonde la Eyasi Wembere, ujenzi wa bomba la kupeleka gesi asilia nchini Uganda, njia ya kusafirisha umeme ya Masaka – Mutukula – Mwanza, pamoja na miradi mingine ya umeme inayotekelezwa mpakani mwa nchi husika.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Katibu Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Haji Janabi, Kamishna wa Petroli na Gesi Adam Zuberi na baadhi ya maafisa waandamizi wa wizara na taasisi zake, walishiriki mkutano huo.

Aidha, sekta nyingine zilizoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Ulinzi na Usalama; Maendeleo ya Miundombinu na Usafirishaji; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Utalii; Kilimo, Uvuvi na Mifugo; Maji na Mazingira; Afya; Elimu na Mafunzo; Habari; pamoja na Utamaduni.

Mkutano ngazi ya Mawaziri ulitanguliwa na ngazi ya Wataalam Septemba 3, ukifuatiwa na Makatibu Wakuu Septemba 4, mwaka huu.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akizungumza wakati wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza – kushoto) akiwa na wajumbe wenzake kutoka Tanzania, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.   
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati-mstari wa mbele), akiwa na baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na wajumbe wengine kutoka Tanzania, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.  

  Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini na Wizara nyingine mbalimbali, wakiwa katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa kwanza kulia-mstari wa mbele), akiwa na wajumbe wenzake kutoka nchi hiyo, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wakiwa katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad