HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 6, 2019

RAIS MUGABE AFARIKI DUNIA

RAIS wa zamani wa nchini Zimbabwe, Robart Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95 huko nchini Singapore alipokuwa akipata matiabu.


Hayati Mugabe aliongoza nchi ya Zimbabwe kuanzia mwaka 1980 hadi 2017 ambapo alipata mrithi wake ambaye ni Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 kwenye koloni la Rhodesia.



Rais Mugabe ambaye alionekana akisema maneno mengi ya masihara katika mtandao ya kijamii na yenye ukweli ndani yake kama  "SOMETIMES YOU LOOK BACK TO YOUR AT GIRLS

 YOU SPEND MONEY ON RATHER IT TO YOUR MUM AND REALISE WITCHCRAFT IS REAL".
Pengine unaweza kusema Mugabe ni Rais aliyekuwa na shahadanyingi kuliko walio wengi, Mugabe alikuwa na shahada saba. Digrii yake ya kwanza alipata kutoka chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini na shahada zake nyinginealisoma kupitia mtandao akiwa gerezani.

Hata hivyo Mugabe alipohojiwa na BBC  Kuhusu afya yake, alisema," Nimekufa mara nyingi hapo ndipo nimemshinda Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja," alisema alipotimiza miaka 88. Ingawa kwa sasa hatuponae tena.

Pia Mugabe wakati wa uhai wake hakuwa mpenzi wa mpira wa miguu  ila baadae utu uzima ulipomfikia alikuwa akiangalia mpira wa miguu na kuwa  hasa  shabiki namba moja wa timu ya Chelsea na Barcelona.


Lakini Mugabe enzi za uhai wake alikuwa mapenzi ya mchezo wa kriketi, akiwa mlezi wa jumuiya ya mchezo wa kriketi nchini Zimbabwe na nyumba na alipokuwa akiishi alikuwa  karibu na uga wa michezo huo huko Harare.


Kuhusu familia yake  Mugabe alikuwa na watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997 wakati huo yeye akiwa na miaka 73, mwaka mmoja baada ya kufunga ndoa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad