MISS TANZANIA KUPATIKANA AGOSTI 23 MWAKA HUU ...MWANUKUZI ATOA NENO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 20 August 2019

MISS TANZANIA KUPATIKANA AGOSTI 23 MWAKA HUU ...MWANUKUZI ATOA NENO

 Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii, ambapo ameeleza kuwa maandalizi yapo tayari na mashindano yatakuwa ya aina take, leo jijini Dar es Salaam.
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MKURUGENZI wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) Basila Mwanukuzi Shayo amesema fainali za mashindano hayo yatahitimishwa rasmi Ijumaa ya Agosti 23 mwaka 2019, ukumbi wa Millenium Tower LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwanukuzi amesema washiriki wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini wapo kambini tangu Agosti 12 mwaka huu wakijiandaa na kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

"Kufanyika kwa fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya Mikoa ambayo yalifanyika kuanzia mwezi April mwaka huu" ameeleza.

Amesema kwa kipindi walichokuwa kambini washiriki wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutembelea, kuwafariji na kucheza michezo mbalimbali na watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

"Washiriki wakiwa kambini wamepata pia nafasi ya kufanya mashindano madogo madogo kwa mujibu wa mashindano ya dunia ambapo walifanya mashindano ya kumtafuta mrembo mwenye kipaji.

"Mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu, na washindi watatangazwa siku ya tukio" ameeleza Mwanukuzi.

Mashindano hayo yanategemewa kuwa ya aina yake ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi zao ili kumshuhudia mlimbwende atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya urembo ya dunia.
 Washiriki wa shindano la Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania nchini, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akiwa na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na warembo hao (waliosimama) leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad