MANARA ATAKA MASHABIKI 60,000 KWA MKAPA SIMBA IKICHEZA DHIDI YA UD SONGO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 20 August 2019

MANARA ATAKA MASHABIKI 60,000 KWA MKAPA SIMBA IKICHEZA DHIDI YA UD SONGO

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MSEMAJI wa timu ya soka ya Simba na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Haji Manara amewaomba wanachama, mshabiki na wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi katika mechi yao ya marudiano dhidi ya timu ya UD Songo itachezwa Agosti 25 mwaka hu kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa maarufu kwa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mbali na kuwahimiza Wana-Simba na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia Simba ,Manara pia amesema anaiombea dua njema timu za Tanzania ambazo nazo zitakuwa na mechi za marudiano ikiwemo timu ya Yanga ambayo amesema anaamini bado ina nafasi ya kusonga mbele.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Manara amewaambia waandishi wa habari kuwa kuhusu maandalizi ya timu yao ya Simba yamekamilika n wachezaji wako tayari kwa mchezo huo na ushindi kwao ni jambo namba moja na si vinginevyo.

"Maandalizi yamekamilika na mechi itachezeshwa na na waamuzi kutoka nchini Rwandwa na viingilio vya mchezo huo ni rafiki kama ilivyo kawaida.Kiingilio kinaanzia Sh.5000, Sh.15,000 na Sh.30,000 wakati Platinum kitakuwa Sh.100,000 na Platinum Plus itakuwa Sh.150,000.

"Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia Alhamisi ya wiki hi kupitia Selcom ambao nao wako tayari kwa kzi hiyo.Kuelekea mchezo huo gari litazunguka katika maeneo mbalimbali yenye mkusanyiko wa watu na tunatarajia kuona mashabiki 60,000 uwanjani na hili kwa Simba sina wasiwasi nalo hata kidogo,"amesema Manara.

Amesisitiza kuwa mashabiki wa Simba ni chachu kubwa ya ushindi wa timu yao na kwamba hata wachezaji wa Simba wakiongozwa na Medie Kagere wamekiri wanapowaona idadi kubwa ya mashabiki uwanjani basi huwa wanapagawa na kuwafanya wacheze kwa moyo wa kujituma ili kushinda mechi.

Hivyo amesema matarajio yao wana Simba watajitokeza kwa wingi kushangilia na ikibidi kuzomea wapinzani wao mwanzo mwisho.

"Nataka kuwaambia msimu uliopita Simba iliongoza kwa kujaza mashabiki wengi uwanjani na matarajio yetu Simba itapata tuzo ya kuingiza mashabiki wengi,"amesema Manara.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mechi itachezwa muda mzuri na siku nzuri ya Jumapili, hivyo mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao."Tunataka mashabiki wa Simba uwanjani hakuna kukaa kimya, muda wote tutashangilia."

Kuhusu kushangilia timu zingine, Manara amewaomba Watanzania kujitokeza kusapoti timu ya KMC na Azam ambao wanatangulia kucheza mechi zao na ni vema uwapa hamasa na kuzishangilia timu hizo na Wana Simba na watanzania wote wajitokeze kwa wingi kushangilia timu hiyo.

Pia amesema ni ngumu kwake kuipenda Yanga na hajawahi kuipenda lakini kwenye mechi yao ya marudiano anaiombea dua ili ishinde kwani kufanya vizuri kwa timu hiyo ni mafanikio kwa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad