HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 20 July 2019

NIMERIDHISHWA NA MRADI WA MAJI WA CHANGANYIKENI- MZEE MKONGEA

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Mbio za Mwenge Kitaifa 2019 zimeridhishwa na mradi wa usambazaji maji wa Makongo-Changanyikeni wenye thamani ya Bilion 75 unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mwenge Mzee Mkongea Ali baada ya kutembelea kituo cha Usambazaji maji (booster Pump) na tenki la kuhifadhia maji.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa na kutembelea maeneo hayo, Mzee Mkongea amesema hizi ni jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kuhakikisha wananchi wote wanapata maji ya uhakika.

"Jitihada zinazofanywa na Rais wetu ni kubwa, tuna mahusiano mazuri na Wenzetu wa India na tumeona katika ripoti fedha walizotupatia kwa ajili ya mradi huu imeondolewa kodi na hilo ni jambo jema kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi," Mkongea.

Amesema, "tulikuwa tukiona kwenye vyombo vya habari kuhusu mradi huu mkubwa na tulipofika na kupitia ripoti tumeona tenki la maji tukaamua kwenda kuliona niwapongeze DAWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia miradi hii,"

Amempongeza pia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo kwa kuweza kusimamia miradi hii mikubwa ya maji ndani ya Wilaya yake.

Kwa upande wa DAWASA, Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huu umekamilika kwa asilimia 76 na umebakia kwenye hatua za mwisho.

Luhemeja amesema kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha Manispaa za Kinondoni na Ubungo na Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo ukiwa unahusisha matenki matano yenye ujazo wa Lita Milioni 6.

Mbizo za mwenge mwaka huu zitetembelea miradi mbalimbali ya Maji ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na kuizindua ikiwa tayari wameshaweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa tanki la maji la Pugu la ujazo wa Lita milion 2 na mradi wa Makongo-Changanyike.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2019 Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe ka Msingi kwenye mradi wa usambazaji maji wa Makongo-Changanyikeni walipotembelea leo Jijini Dar es salaam.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2019 Mzee Mkongea Ali akizungumza baada ya kutembelea mradi wa usambazaji maji wa Makongo- Changanyikeni na kuridhishwa na mradi huo ulipofikia na kuwapongeza DAWASA kwa kuweza kusimamia mpaka hapo ulipofikia. Mwenge huo utatembelea miradi mbalimbali inayosimamiwana mamlaka hiyo.
 Afisa Mtendaji Mkuu ww DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akielezea ramani ya mradi wa usambazaji maji wa Makongo-Changanyikeni wenye thamani ya bilioni 75 utakaohudumia wakazi wa Wilaya ya Kinondoni, Ubungo na Mji wa Bagamoyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakisikiliza jambo kutoka kwa Kaimu Meneja miradi wa Maji Ramadhani Mtindasi wakati wa Mbio za Mwenge zilipotembelea mradi wa usambazaji maji Makongo Changanyikeni.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2019 Mzee Mkongea Ali alipotembelea tanki la maji lamradi wa usambazaji maji wa Makongo-Changanyikeni walipotembelea leo Jijini Dar es salaam

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad