HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 19 July 2019

KIONGOZI WA MWENGE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA TENKI LA MAJI PUGU

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali ameweka jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa tanki na mfumo wa usambazaji maji katika maeneo ya Pugu, Gongo la Mboto, Pugu Station, Air Wing, Ukonga na Majohe.

Kiongozi huyo pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mgema kuhakikisha malighafi zote zinazotumika katika mradi wa maji Pugu yanafanyiwa vipimo kubaini ubora wake ili kuhakikisha mradi huo unakuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi huo ambao unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam DAWASA.

Mmradi huo umegharimu Sh. Bilioni 7.3 ambapo Mzee Mkongea amemshukuru Rais Magufuli kwa  kuhakikisha watu wanapata MajiSafi na salama.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa  mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huo unatekelezwa na mamlaka hiyo ikiwa ni katika jitihada za kuboresha huduma za maji kwenye maeneo yaliyokuwa hayana mtandao wa maji safi lengo ni kufikia asilimia 95 ya wakazi mnamo 2020.

"Mradi huu unatarajiwa kusambaza maji katika maeneo ya Pugu, Majohe, Gongo la mboto, Bangulo, Ukonga-Airwing, Kigogo na Buyuni/Chanika na maeneo jirani pia mradi utaendelea kupanuliwa kulingana na upatikanaji wa fedha", amesema

Ameongeza kuwa bomba Kuu litakuwa na uwezo wa kusafirisha kiwango cha maji kipatacho lita 2,880,000 kwa siku ambapo wakazi wapatao 450,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo pamoja na maunganisho mapya ya wateja zaidi ya 50,000 yatafanyika mara baada ya kukamilika kwa mradi. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akisoma risala wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uwekaji wa  jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha namna  mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto utakavyofanya kwa Viongozi wa Mbio za mwenge mwaka 2019.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad