HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 18, 2019

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUSAJILI BIASHARA ZAO

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

Wakala wa usajili wa biashara na leseni nchini( BRELA)  wamewakutanisha wadau mbalimbali wa biashara Mkoani Arusha,lengo likiwa ni kuwapa mwongozo wa kampuni kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao( ORS)

Akizungumza wakati wa semina inayoendelea Jijini Arusha Mkurugenzi wa fedha na utawala Tanzania Bakari Ally Mketo amesema kuwa kuna umuhimu wa kutambulisha Mfumo huo kwa wafanyabiashara ili kuweza kufanya Kazi kwa uweledi na ufanisi .

Aidha amesema kuwa mwamko wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao.

Alibainisha kuwa hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni yatakayojisajili

" malengo yetu ni kuhakikisha tunapanua wigo mpana na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo"alisema mketo

Nao baadhi Ya wafanyabiashara waliyohudhuria kwenye semina hiyo akiwemo Privanus Saimon na John Tasha wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizonazo hivyo watafanya maboresho ya leseni zao ili waweze kuendesha makampuni yao kwa uhuru

Walisema kuwa kabla ya semina hiyo walikuwa Hawafahamu mambo mengi lakini tangu wapewe mafunzo hayo wameelewa na wamejua umuimu wa kusajili majina yao ya biashara pamoja na kubaini faida zakutoa taarifa Kwa mamlaka husika pindi wanapo funga biashara Zao

Alisema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa hawajui faida za kutoa taarifa pindi wanapofunga biashara zao, kwani wamekuwa hawana elimu juu ya faida na hasara za kutoa elimu hivyo waliomba brela kuendelea kutoa elimu ili wananchi wengine ambao hawajui waweze kufahamu 

Waliiomba serikali kufuta madeni yote ya nyuma ambayo wananchi hao ambao ni wafanyabiashara waliokuwa wamesajili majina yao brela na teari wamefunga biashara lakini hawakutoa taarifa katika vyombo husika kitendo kilichowapelekea kuwa na mlimbikano wa madeni makubwa na mengi ili waweze kuanza upya kwani kwasasa wamepewa elimu na wataendelea kuwapa elimu wefanya biashara wengine 

"unajua unakuta mfanyabiashara kama Mimi nimesajili biashara yangu au jina la biashara brela ,nikasajili mamlaka yamapato na nimeendesha biashara mwishowe nikafunga labda kutokana nakukosa mtaji wa biashara au la nanilipofunga sikuwa najua kuwa natakiwa kutoa taarifa kitendo kinachonipelekea kulimbukiwa madeni kila siku na Mimi sijui kama nilivyofunga nilitakiwa kutoa taarifa kitu ambacho nichangamoto kubwa sana kwangu na yote hii imesababisha kutokana na awali kutokuwa na elimu "John Tasha

Kwa upande wake mmiliki ubunifu wa BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo amesema mfumo huo utasaidia kukamilisha usajili kwa haraka na kupunguza gharama kubwa ambazo wafanyabiashara walikuwa wanatumia

"Katika mfumo wa OBS wananchi haswa wa mkoani hususa ni Arusha walikuwa wanatumia mda mwingi mpaka kusajili pia walikuwa wanatumia fedha nyingi sana kwani walikuwa mpaka wasafiri ndio wasajiliwe lakini kwa mfumo huu mpya wa ORS ambao ni mfumo ambao Mwananchi ambaye ni mfanya biashara atajisajili kupitia njia ya mtandao "alisema Suzana

“Kwa kweli niwaambie wakazi wa mkoa huu wa Arusha na mikoa ya jirani wachangamkie fursa hii ya kuweza kutumia muda huu kuweza kusajili majina ya biashara zao, makampuni na nembo lakini pia leseni daraja A zililokuwa zinasajiliwa Wizara zimerudishwa kwetu na hivyo pia wanasajili iwapo walengwa watakidhi vigezo vilivyowekwa “Alisema 

Aidha alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kusajili ili kuweza kusajili kampuni lakini lazima vigezo na masharti husika vinavyohitajika kwenye upatikanaji wa leseni hiyolazimauzingatiwe 

Alisema kuwa kwakufanya hivyo kutawasaidia kuongeza kiwango cha biashara Zai kwani akiwa amesajili jina na kampuni itakuwa inatambulika kimataifa zaidi. 
Mmiliki Ubunifu wa  BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo akitoa Elimu kwa washiriki hao. 
 Mkurugenzi wa fedha na utawala Tanzania Bakari Ally Mketo akiongea na waandishi WA habari katika semina hiyo  
26Picha ikionyesha washiriki wakifuatilia mafunzo kwa makini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad