TCRA yafunika kampeni ya Mnada kwa Mnada mkoani Kilimanjaro katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 28 June 2019

TCRA yafunika kampeni ya Mnada kwa Mnada mkoani Kilimanjaro katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini  Julius Felix  amesema ni fursa kwa wananchi wa Kilimanjaro kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano. 

Felix mesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. 
"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema ni fursa kwa wananchi wa Kilimanjaro kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano. 

Amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. 
"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" Felix
 Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Doris Muhimbila akitoa maelezo kwa wananchi wakati kampeni ya Mnada kwa Mnada mkoani Kilimanjaro.
 Afisa wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandao akitoa maelezo kwa mwananchi kuhusiana na makosa ya mtandaoni yanayotokana na matumizi mabaya ya simu.
 Wananchi wakipata huduma mbalimbali katika kampeni ya Mnada Kwa Mnada inavyoendeshwa na TCRA.
Afisa Kusajili wa NIDA Mkoani wa Kilimanjaro Abubakar  kalinga akitoa maelezo wakati wananchi waliofika katika kampeni ya TCRA ya Mnada kwa Mnada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad