Meneja Mkuu wa taasisi ya 'Wefarm' Bw. Nicholus John akizungumza na wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi ya We Farm Bi. Cyrila Anton (picha ya juu) akitoa ufafanuzi zaidi masuala mbalimbali ya wakulima.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Taasisi ya 'WEFARM' imezinduliwa itakayowawezesha wakulima kubadilishana taarifa kwa njia za kidigitali.
Akizungumza na wanahabari wakati akizindua jukwaa la wakulima,Mkurugenzi Msaidizi wa Uinuaji wa Mazao, Pembejeo na Ushirika wa Wizara ya Kilimo Bw. Beatus Malema
Amesema malengo ya serikali yetu nikuweza kufanya kazi pamoja na sekta binafsi, serikali za mitaa na watoa huduma wanaotoa huduma bora katika sekta ya Kilimo.
"Tunakaribisha Wefarm naninaimani kuwa mmekwenda kwa wahusika katika sekta ya kilimo na wamewasaidia kujua changamoto zinazo wakabili," amesema Bw. Beatus Malema.
"Jukwaa la Wefarm limetengenezwa kwa uwazi na litawawezesha wakulima toka pande zote za Tanzania kuweza kupata elimu, maarifa, kupashana habari na kutatua matatizo ili kuuza bidhaa zilizo bora." amesema Bw. Malema.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa WE FARM , Bw.Nicholaus John alisema huduma hiyo ni bure na mkulima atatuma ujumbe mfupi kupitia namba 15088.
“Mkulima ataweza kuuliza maswali na kupata majibu kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo shambani wkake, wazo hili lilikuja kutokana na kwamba wakulima wanachangamoto nyingin mashambani lakini wanakosa habari au ujuzi wa kuweza utatua matatizo yao.
No comments:
Post a Comment