*Usajili wa laini za Airtel kwa kutumia alama za vidole ni
BURE kwa wote.
Dar es Salaam Alhamisi 2 Mei 2019 … Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel Tanzania imetangaza maduka ya Airtel maoney Branch kila kona
rasmi kusajili laini za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya
kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole kwa mteja
walioko kila mkoa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuanza kwa zoezi hilo, Meneja
Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Kama utakumbuka
mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilizindua mfumo huu
kwa majaribio. TCRA pia siku hiyo ilitoa mwongozo kwa makampuni yote
ya simu kuweka utaratibu na kufanya usajili wa laini za simu mpya kwa
kutumia mfumo huu mpya katika maeneo ya mikoa sita ya majaribio. Baada
la zoezi hilo serikali ilitoa taarifa za kuanza usajili kwa kutumia
alama za vidole kwa wateja wote. Leo hii Airtel Tanzania tunatangaza
rasmi kuanza kwa zoezi hili kwenye Airtel Money Branch zaidi ya 600
pamoja na maduka ya Airtel yote bila gharama yoyote yaani BURE”
“Usajili huu wakisasa unaotumia alama za vidole ni wa uhakika zaidi
na vigumu kughushi, ni muhimu sana wateja wote wapya ambao wanajiunga
na Airtel kwa sasa kusaijili kwa mfumo huu’ alisema Mmbando.
Vile vile Airtel itaweka vituo maalum kwenye maeneo ya taasisi za
serikali na ofisi za makampuni mbalimbali kurahizisha zoezi hili.
Kadhalika, makampuni na taasisi zinaweza kuomba kutembelewa na Kitengo
cha huduma kwa wateja Airtel ili kufanyiwa usajili kwenye maeneo yao
ya kazi kwa kuwa sisi tunathamini muda wa wateja wetu tutajipanga na
tutakwenda’ alisema Mmbando.
“Wateja wetu hasa wale wa zamani tunawasihi kuhakiki taarifa zenu za
usajili kwa kupiga *106# endapo taarifa zako za usajili haziko sahihi
tembelea duka letu lililopo karibu yako ili kukamilisha usajili wako
kwa kutumia mfumo huu mpya wa kutumia alama za vidole” aliongeza
Mmbando.
“Tunasisitiza Usajili huu ni bure na unaendelea kwenye Airtel Money
Branch zote na maduka yote ya Airtel, mteja anachotakiwa kuwa nacho
ili kusajili ni kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kutoka
NIDA, alisema Mmbando
Tunaendelea kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari
yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa
ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi
ya 600 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani yetu
tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kadri muda unavyokwenda.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanaotumia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel wakifanya usajili katika makao Makuu kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na utaendelea hadi Decemba mwaka huu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson MMbando akiongea na baadhi ya wateja
waliojitokeza jana katika maduka ya Airtel ili kusajili laini zao kwa
alama za vidole na kuwashauri kutembelea pia maduka ya Airtel huduma
kwa mteja zaidi ya 20yalioko popote karibu nao pamoja na Airtel Money
branch zaidi ya 600. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na
utaendelea hadi Decemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment