HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 2 May 2019

MAKATIBU WAKUU TANZANIA NA UGANDA WAHITIMISHA MKUTANO WA MAHUSIANO NA KUSAINI MAKUBALIANO

Na Munir Shemweta, BUKOBA

Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, Kiuchumi na Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot kusaini makubaliano yaliyofikiwa.

Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi za Tanzania na Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo mbili walikutana na kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda katika eneo la Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu kwa lengo la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel alisema katika siku mbili za mkutano huo, nchi washiriki zilijadili namna bora ya kuendeleza mahusiano ya mipakani kwa lengo la kurahisisha mambo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira sambamba na kujadili jinsi ya kuboresha matumizi endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera ili ziweze kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Okidi Ollot alisema, mkutano huo ni njia sahihi ya kuonesha kuimarika kwa mahusiano ya Tanzania na Uganda na kusisitiza kuwa kilichofanyika ni kuonesha uhalisia wa ushirikiano kwa lengo la kuwafanya wananchi wa pande zote kunufaika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru pande zote mbili za nchi za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano aliyoyaeleza kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot baada ya kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot wakionesha hati za makubaliano baada ya kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot (Wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani Kagera. (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa kwanza kulia) na Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa kufungwa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani Kagera.
 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
 Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima akizungumza kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WA WIZARA YA ARDHI)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad