HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 17, 2019

ZIARA YA RC MAKONDA YAZIDI KUIBUA MADUDU UJENZI WA BARABARA

*Afurahishwa na ujenzi wa ofisi za walimu kwa hisani ya mkandarasi Madale

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

ZIARA ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda imeendelea kwa kutembelea Manispaa ya Kinondoni na kukagua miradi ya kimaendeleo huku akiibua ubadhirifu mkubwa wa fedha unaofanywa katika miradi hiyo hasa barabara.

Akikagua barabara ya Kilonga wima inayojengwa kwa hisani ya benki ya dunia Makonda amegundua fedha ya ziada takribani shilingi milioni 800 inayotumiwa na kandarasi hiyo ukilinganisha na barabara zinazosimamiwa na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA)

Mshauri wa mradi mhandisi Henry Ngogolo amemweleza mkuu wa Mkoa kuwa barabara hiyo inajengwa kwa shilingi bilioni 2.5 kwa kilometa huku TARURA wakijenga barabara za kilometa hizo kwa shilingi bilioni 1.5.

Makonda amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kutafuta namna kuhusiana na ujenzi wa barabara za jiji hilo hasa katika usimamizi na washauri wa miradi hiyo ili kuweza kuokoa fedha na kusaidia wananchi kutatua kero nyingine na sio kurundika fedha kwenye mradi mmoja ambao bado hautekelezwi vizuri.

Aidha Makonda ametembelea na kukagua ujenzi barabara ya Salasala iliyosimamiwa na TARURA na imekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 900 kwa mita 700 walizopatiwa kwa matengenezo.

Pia akiwa Salasala amekutana wananchi ambao walieleza hofu zao za kubomolewa nyumba zao ambazo zimepita katika mkondo wa maji na reli na RC Makonda amewatoa hofu kwa kuahidi kushughulikia suala hilo.

Aidha ziara yake imemulika katika Shule ya Sekondari ya Kisauke Madale ambayo ilikuwa na changamoto ya kukosa ofisi za walimu na vyoo hali iliyopelekea walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.

Akiwa shuleni hapo Makonda amefurahishwa kasi ya ujenzi wa ofisi za kisasa kwa ajili ya walimu zinayojengwa na kandarasi inayojenga barabara ya Goba, Madale hadi Wazo bure ikiwa ni mchango wao katika kusaidia sekta elimu.

"Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza mazingira ya utendaji kazi kwa walimu yalinihuzunisha, hasa kwa kukosa ofisi na kuchangia vyoo na wanafunzi, na nilimwomba mkandarasi anayekarabati barabara ya Goba Madale awaangalie kwa hilo na ninafurahi kwa kazi nzuri na ya mfano inayofanywa na kandarasi hii" ameeleza Makonda.

Aidha amewataka wanafunzi kuangalia malengo yao na kuweka nidhamu mbele ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao ambapo kupitia mkuu wa shule hiyo Fadhili Mutarubukwa wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa moyo na uthubutu wa kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili tangu mwaka 2009 na wamehaidi kutokomeza  daraja sifuri katika matokeo ya kidato cha nne ili kuonesha thamani ya elimu bure inayotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kisauke iliyopo Madale jijini humo ambapo amewataka wazingatie masomo yao na kuwa na nidhamu kwa walimu wao, jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa maelekezo kwa viongozi alioambatana nao mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Salasala na kuzungumza na wananchi waliotoa kero zao hasa hofu ya kubomolewa nyumba zao, jijini Dar es Salaam.
Muonekano ya barabara ya Salasala jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad