HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 17 April 2019

BUNGE KUISHAURI SERIKALI KUTEKELEZA AZIMIO LA MALABO KUTENGA ASILIMIA 10 KWENYE BAJETI YA KILIMO

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa bunge limejipanga kuishauri serikali kutekeleza azimio la Malabo la kutenga Asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya usalama wa chakula na suala la lishe bora kwa jamii.

Akizindua jukwaa la majadiliano ya Usalama wa chakula ya mabunge ya Afika mashariki na kusini iliyoandaliwa na Bunge la Afrika mashariki Ndugai alisema kuwa changamoto kubwa kwenye sekta ya kilimo bado bajeti yake haijatekelezwa kwa asilimia japo 30 hivyo kwa kuanzia angalau kwenye bajeti za maendeleo za nchi zetu tukaanzia na asilimia 10

Amesema kuwa pamoja na serikali kujitahidi bado kunachangamoto kubwa ya lishe duni na udumavu katika jamii hivyo kama tunataka kufikia kwenye maendeleo ya kiuchumi tunahitajika kujenga miundombinu ya kufikika kwa wakulima wetu sanjari na kuhimiza kilimo na ufugaji kwa kutenga bajeti inayoakisi kufikia huko.

“Changamoto ninaoyoiona leo kwetu kama nchi za bara la afrika ni kutoona umuhimu wa kujipanga kutekeleza azimio la Malabo baada ya viongozi wetu wa mataifa ya bara hili kuipitisha mwaka 2014 kuhusu usalama wa chakula hivyo muhimu kama nchi zetu kuweka maazimio kama mabunge linalotaka kila nchi kwenye bajeti yake ikaweka asilimia 10 kwa ajili ya sekta ya kilimo mifugo na uvuvi”alisisitiza Ndugai.

Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Asha Abdallah Juma(Mshuwa)ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuwa na usalama wa chakula ili kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto kwa kukosa lishe bora kwenye miaka mitatu ya mwanzo.

Amewataka wa Bunge kutotunga Sheria pekee na wajikite kuwa na mashamba ya mfano Kwa wananchi wanaowaongoza kuibua uzalishaji na kilimo kikue hapo tutapata maendeleo ya kiuchumi.

"Sisi Kwa mfano tulianzisha chuo maeneo ya chukwani Kwa lengo la kuwezesha jamii kutumia eneo dogo kuzalisha Kwa tija ili tunapopata nafasi tuitumie vizuri kuzalisha chakula Kwa wingi"

Mshuwa alieleza kuwa warsha hizo ni nzuri Sana kwani zinasaidia nchi zetu kuondoa changamoto zinazotukabili ikiwemo ukosefu wa Ardhi Kwa ajili ya uzalishaji inayotufanya kutokuwa na usalama wa chakuli na lishe duni.

Nae mbunge wa Babati vijijini Jituson alisema kuwa mkoa wa Manyara ni wazalishaji wakubwa lakini udumavu bado ni changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa lishe Bora Kwa watoto wanaozaliwa hivyo kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuongeza bajeti yetu kwenye kilimo mifugo na uvuvi.

Ameitaka jamii kurudi Kula vyakula vya asili ambavyo havina wanga mwingi na kuacha Kula vyakula ambavyo vitasababisha miili kukosa afya Bora.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad