HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 17 April 2019

TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

VICTOR MASANGU, KIBAHA

VIJANA wapatao 35 katika halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani ambao walikuwa wanakabiliwa na wimbi la ukosefu wa upatikanaji wa ajira wamepatiwa mafunzo maalumu ya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na tatizo la umasikini.

Hayo wamebainishwa na Meneja wa Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna Manuti wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku 11 ya ujasiliamali kwa baadhi ya vijana waliopo katika halmashauri ya mji Kibaha ambayo yameandaliwa kwa lengo la kuwapa mbinu mbali mbali zitakazoweza kuwasaidia kujiajiri na kuacha na kuwa tegemezi.

Aidha Meneja huyo amebainisha kuwa katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana wameamua kuwakutanisha vijana hao kwa lengo la kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ambayo itawapa fursa ya kuanzisha biashara zao wenyewe lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

“Hii programu ya kuwawezesha vijana mafunzo ya ujasiriamali tunaifanya kwa kipindi cha miaka miaka mine na inatarajia kumalizika mwaka 2020 na kwa sasa huu ni mzunguko wa sita ambapo katika halmashauri ya mji wa kibaha vijana wapatao 35 wamepata fursa ya kupatiwa mafunzo haya ambayo yatawea kuwasaidia kuweza kujiajiri wao wenyewe,”alisema Anna.

Kwa upande wake Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga amesema programu ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali itawasaidia vijana kujiajiri wao wenyewe kutokana kuanzisha viwanda vidogovidogo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kupambana na wimbi la umasikini.

“Kwa kweli mradi huu wa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana hasa katika Mkoa wetu wa Pwani na sisis kama Sido tutahakikisha tunashirikiana bega kwa beda na taasisi hii ya TECC ambayo imefanikisha kuwakusanya vijana hawa na kuwapa mahalifa ambayo yatawasaidia kupata ajira pamoja na kuanzisha viwanda vidogividogo,”alisema Mlinga.

Nao baadhi ya vijana ambao wameshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Selemani Shabani pamoja na Azaria Namga wamesema kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na ajira, ukosefu wa mitaji ya biashara hivyo wameiomba serikali ya awamu yatano kuwasaidia kwa halina mali ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.

MRADI huo wa kuwawezesha vijana kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali unatekelezwa katika mikoa mine ya Jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara pamoja na Pwani ambapo hadi sasa katika mikoa yote hiyo vijana wapatao 894 wamenufaika na programu hiyo ambayo inatarajia kumalizika mwaka 2020.
Meneja wa Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna Manuti akizungumza jambo na vijana ambao wameshiriki wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya ujasiliamali ambayo yamefanyika katika katika kata ya maili moja Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU) 
Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga akizungumza jambo katika ufunguzi wa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana wa halmashauri ya mji Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU) 
Mmoja wa wawakilishi wa vijana kutoka katika halmashauri ya mji Kibaha Shauri Yomba Yomba akizungumza na washiriki ambao hawapo pichani kuhusiana na umuhimu wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yameandaliwa na taasisis ya TECC(PICHA NA VICTOR MASANGU) 
 Mwezeshaji wa semina hiyo ambaye pia ni Afisa kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Merina Mkuchu akitoa maelekezo kwa vijana hao ambao wameshirki katika mafunzo ya ujasiriamali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya vijana kutoka katika halmashauri ya mji Kibaha ambao wameshiriki katika mafunzo ya ujasiriamali wakiwa wanasikiliza mada ambazo zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji kutoka TECC pamoja na SIDO.(PICHA NA VICTOR MASANGU.)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad