HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 April 2019

WALIOTUMIA JINA LA MAMA JANETH MAGUFULI KUTAPELI WAPANDISHWA KIZIMBANI

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WATU saba wakazi wa jijjini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu wanne tofauti wakikabiliwa na mashtaka mbali mbali likiwemo la kuchapisha taariza za uongo katika mtandao wa kijamii wa face book kwa kutumia jina la Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magifuli, mama Janeth Magufuli.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, Wanjah Hamza, Augustine Rwizile na Janet Mtega.

Akisomahati ya mashtaka wakili wa serikali Batlida Mushi amewataja washtakiwa hao kuwa ni,  Saada Uledi, Maftaha Shaban, Heshima Ally, Shamba Baila,Fadhili Mahenge, Obadia Kwitega na Stella Ommary.


Mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa kuwa, Kati ya January 2017 na Machi 2019 jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa  Saada, Shaban, Ally na Baila walikula njama ya kuchapisha maneno au taarifa za uongo kupitia ukurasa wao wa Facebook.

Katika shtaka la pili imedaiwa washtakiwa hao walichapisha machapisho katika ukurasa wao wa Facebook kuwa, Janet Magufuli ambaye ni mke wa Rais Magufuli ameunda Taasisi inayofanya kazi ya kukopesha  na kutoa mkopo kwa watu ikiwa na masharti yanayowataka watu hao kuweka fedha kama dhamana ya kupata mkopo huo.

Katika shtaka la tatu imedaiwa, kati ya Machi 2 na machine 8, 2019 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa kama waendeshaji wa ukurasa wa Facebook iliyosajiliwa kwa jina la Janeth Magufuli, kwa nia ya kudanganya na kupotosha na kwa kutumia mahamisho ya fedha kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine walijipatia  sh. Milioni 4,487,000/- kutoka kwa Simon Kunambi kama ulinzi/ dhamana ya mkopo ambao angepatiwa kutoka kwenye hiyo Taasisi ya Janeth Magufuli, huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la nne, imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha huku wakijua fedha hizo in zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza imedaiwa kati ya Januari 2017 na Machi 2019   mshtakiwa Mahenge akiwa Dar es Salaam, Rukwa, Mkoani Songwe na sehemu zingine za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alisambaza taarifa za uongo kwa kutumia ujumbe wa tuma pesa kwenye namba hii huku akijua ujumbe huo ni wa uongo uliokuwa na nia ya kupotosha umma.
Mshtakiwa Huyo pia anadaiwa katika siku na mahali hapo, alianzisha na kusambaza ujumbe bila radhaa ya mpokeaji kwa kutumia laini za simu ambazo amezisajili kwa jina lake kupitia mitandao tofauti tofauti.
Aidha mshtakiwa huyo anadaiwa  akiwa ndani ya Tanzania na nje ya nchi alisambaza ujumbe kwa watu mbali mbali kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia mshtakiwa Mahenge anadaiwa kwa  njia ya udanganyifu kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia laini zipatazo 629 ambazo zilikuwa zimesajiliwa kwa jina lake alijipatia sh. Milioni 123 kutoka kwa watu mbali mbali huku akijua analolifanya siyo la kweli.

 Aiidha mshtakiwa  anadaiwa kutakatisha fedha kwa kujipatia sh. milioni 123 huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi, washtakiwa wamerudishwa rumande. Kesi hiyo itatajwa tens Mei 2, mwaka huu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Janet Mtega imedaiwa siku mshtakiwa Obadia Kwitega aliendesha Televisheni kwa njia ya mtandao bila kibali.

Imedaiwa kati ya Januari ,29 2017 na Machi 29 2019, jijini Dar es Salaam,  mshtakiwa kupitia Televisheni ya Mtandaoni ya  Bongo Time, alitoa matangazo bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA.
 Pia mshtakiwa huyo anadaiwa Kati ya Februari 22 na Machi 29, 2019 alichapisha  habari ya uongo isemayo Warioba bila ya uoga Tundu Lisu akiwa Rais tutegemee haya, alifanya hayo huku akijua kwamba hana kibali kutoka TCRA.

Mashtakiwa huyo amekana kutenda makosa hayo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshtakiwa kusaini bondi ya sh. Milioni tatu na kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. Milioni tatu. Kesi huyo itatajwa tena April I.
Mbele ya Hakimu Mkazi,Augustine Rwizile imedaiwa, kati ya Januari ,29 2017 na Machi 29 2019, katika sehemu mbali mbali jijini Dar es Salaam,  mshtakiwa Obadia Kwitega na Stella Ommary, kupitia Televisheni ya Habari Mpya ya mtandaoni, walitoa matangazo bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA.
Kesi huyo itatajwa tens Aprili 30, mwaka huu.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad