HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 18, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2019


 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi yake wakati wa kikao cha uchaguzi wa mfanyakazi bora kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akifafanua jambo kwa watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge.
 Baadhi ya wafanyakazi bora wa Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akisimamia zoezi la kuhesabu kura kwa ajili ya kumchagua wa mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni wawakilishi wa wafanyakazi bora walioingia kwenye ushindani.
 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimpa mkono wa pongezi mfanyakazi bora wa mwaka 2019 wa ofisi yake Bw. Jafari Kalaghe, Afisa Tawala baada ya uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
 Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akitoa ufafanuzi wa kanuni za kumchagua mfanyakazi bora kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni  Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Musa Joseph.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa tayari kuwasilisha kura yake baada ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni  Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw Ayoub Banzi na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Mary Mwakapenda.

 Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsilikiza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) alipokuwa akitangaza mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Utumishi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imefanya uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa mwaka 2019 kwa kuwashindanisha wafanyakazi bora saba (7) kutoka Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ambao wamepatikana kwa kigezo cha utendaji kazi mzuri kupitia Mfumo wa Wazi wa Mapitio ya Utendaji Kazi (OPRAS).

Mfanyakazi bora aliyechaguliwa ni Afisa Tawala, Bw. Jafari Kalaghe kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu. 
Mara baada ya kumtangaza Bw. Kalaghe kuwa mfanyakazi bora, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba, amempongeza kwa ushindi na kuwashukuru watumishi kwa kufanya uchaguzi uliozingatia vigezo.

Bw. Kiliba amesema kuwa, Bw. Kalaghe ni mchapakazi hodari anayeonekana na kila mtu na amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza kabla ya uchaguzi, Bw. Kiliba, aliwataka watumishi kumchagua mtumishi ambaye utendaji kazi wake unaonekana kuwa ni bora badala ya kuchagua kwasababu za kufahamiana.

“Tunapopiga kura, tusimchague mtumishi kwasababu unamfahamu au anatoka kwenye idara au kitengo kimoja, bali tumchague kwa uchapakazi wake unaoendana na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, inayohimizwa na Serikali ya Awamu ya Tano,” Bw. Kiliba ameongeza.
Kwa upande wake, mfanyakazi bora aliyechaguliwa, Bw. Jafari Kalaghe amewashukuru watumishi kwa kuona utendaji wake na kuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad