HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 24 April 2019

UVCCM YAKANUSHA TUHUMA ZA KUMFUKUZISHA KAZI DAKTARI ARUSHA

Na Vero Ignatus

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Arusha Mjini Saipulani Abdallah Ramsey amekanusha vikali taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa CCM imemfukuza kazi mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Ngarenaro.

Akizungumza na Vyombo vya habari jijini Arusha Ramsey amesema kuwa kilichofanywa na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM kata ya Levolosi ni kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Aidha alisema kuwa ipo mitandao ya kijamii iliyotoa taarifa hiyo na kusema ccm imemfukuza kazi daktari huku  swala hilo likizua mjadala kwa jamii nzima.

"Alichokifanya mwenezi ni kusimamia utekelezaji na ndio kazi yetu sisi kama chama tawala alifika katika kituo cha afya Ngarenaro na kukuta hakuna huduma na kumtafuta daktari ambaye hakuwapo pia katika eneo hilo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma na malalamiko hapo mengi tu na sio kiki za kisiasa muelewe hivyo" alisema Ramsey

Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema kuwa ccm haimfukuzi mtu kazi Bali kusimamia mienendo mizima ya uwajibikaji na watanzania wanapata huduma. Alisema kuwa wanashangaa namna ambavyo mjadala huo unakuwa makubwa wakati kazi yao ni kuhoji wataalamu.

Itakumbukwa kuwa ipo video clip ambayo inasambaa mitandaoni kumuonesha katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho akiwasiliana na mganga mfawidhi wa kituo hicho akimtaka kufika kituoni hapo,na mganga huyo kudai kuwa hawezi kufika yupo mbali shambani ambapo tukio hilo pia limesababisha mkurugenzi wa jiji la Arusha Daktari Maulid Madeni kumvua nafasi hiyo na kubaki kuwa daktari wa kawaida.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini Saipulani Abdallah Ramsey .

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad