HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 5, 2019

DC JOKATE AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUJITOLEA MILIONI 915/- KAMPENI YA TOKOMEZA ZIRO KISARAWE

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza jambo mbele ya Waananchi na Wanafunzi kabla ya kupanda mti kwenye eneo ambalo ujenzi wa shule hiyo ya kisasa na ya mfano itajengwa huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Kibuta kwa kukubali kufanyika kwa ujenzi huo ambapo wamekubali kutoa eneo bure.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawa Jokate Mwegelo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana ofisini kwake alipokuwa akieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye kampeni ya kuhamasisha harambee ya kuchangia Tokomeza Zero Kisarawe ,Jakate akionekana mwenye bashasha na furaha muda wote alieleza kuwa kampeni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.Joketi alisema kuwa uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wengine.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari jana alipokuwa akitoa mrejesho kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwakwe Kisarawe,fedha na ahadi zilizopatikana wakati wa hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawa Jokate Mwegelo akiwashukuru Waandishi wa habari pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa kuhamasisha harambee ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe ,ambapo alieleza kuwa kampeni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.Joketi alisema kuwa uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wengine.
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Joketi Mwegelo, sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakitoa mrejesho wa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo iliyojulikana kwa jina la Tokomeza Zero Kisarawe,iliyofanyika wiki iliopita ndani ya Mlimani City,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani,Mh. Jokate Mwegelo akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari jana alipokutana na jana wakati akitoa mrejesho wa fedha na ahadi zilizopatikana kwenye hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Kisarawe,Musa Gama akieleza namna fedha hizo zilizopataikana katika harambee hiyo,zitakavyosaidia kutokomeza zero wilayani hummo, amesema shule itakayojengwa itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita,na kwamba itakuwa ya mfano na itasaidia kuongeza ufaulu wa Wanafanzi kwa kiwango kikubwa. ''Jambo tunaloenda kulifanya ni shirikishi ndio maana tunaungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo wananchi waliojitolea ardhi kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili kuongeza kiwango cha ufaulu”alisema Gama huku DC Jokate akimtazama kwa tabasamu zuri la mafanikio hayo.
DC Jokate akimsikiliza kwa makini mmoja wa Waandishi kutoka Chanell Ten,Said Makalla (aliyenyoosha mikono kulia),alipoulizwa moja ya swali kuhusiana na mafanikio makubwa ya Harambee hiyo ya kutokomeza zero wilani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani,Mh. Jokate Mwegelo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana,wakati alipokuwa akitoa mrejesho kuhusu fedha na ahadi zilizopatikana wakati wa hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Kisarawe,Musa Gama
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa amelinyanyua tofali la saruji na kulitupa chini kuhakiki ubora wake wakati akiwaonesha waandishi wa habari mradi huo ambao unaendeshwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule mbalimbali na miundombinu mingine katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akionesha mradi wa matofali unaoendelea kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya bweni kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na shule zingine.PICHA NA MICHUZI JR.


*Ni katika kufanikisha ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kisarawe ...

Kauli ya DC Jocate yawakuna wananchi eneo ambalo shule inajengwa Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo, ameeleza kuwa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.

Uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na Jocate kwa kushirikiana na viongozi wengine.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mwegelo amesema baada ya kuzindua harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi huo wameamua leo kutoa mrejesho kwa Watanzania wa nini ambacho kimepatikana.

",Tumefanikiwa kukusanya Sh. milioni 915 kati ya Sh. bilioni 1.3 tulizolenga kukusanya.Fedha taslimu ambazo zimeshawekwa benki hadi jana ni Sh. milioni 80 na bado tumeendelea kupokea ahadi za wadau mbalimbali wanaotaka kuchagia.

" Mbali na michango ya fedha tuliyopokea, Chama cha Wahandisi Wanawake, wamejitokeza kutoa ushauri wa namna ya kujenga mabweni hayo.Pia amesema wapo wadau waliochangia mabweni mawili yanayochukua wanafunzi 80 kila moja na lengo ni kujenga mabweni sita,"amesema Jocate.

Amesema anawashukuru wananchi wa Tanzania na wadau wa maendeleo waliojetokeza kuchangia kampeni hiyo ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu, ingawa kwa siku za usoni watajenga na ya watoto wa kiume kwani kupanga ni kuchagua.

“Kama mnavyojua Machi ulikuwa mwezi wa wanawake, Wilaya ya Kisarawe tukaona badala ya kuvaa sare na kusherehekea ni bora tuwe na kampeni itakayoinua wanawake wengi wa kesho ambao ni wanafunzi wa wilaya yetu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowafanya kushindwa kufikia malengo yao,"amesema.

Pia amesema Kampuni ya Sao Hill wamejitolea kutoa mbao za kuezeka mabweni hayo zenye gharama ya Sh. milioni 10 na kutoa mafunzo ya ufundi wa kutengeneza samani kwa mgambo 40 wa wilaya hiyo.Ameitaja misaada mingine waliyopokea ni mifuko 1,890 ya saruji na tayari 1,050 imeshapokelewa ofisini kwake na kontena moja la marumaru.

“Pamoja na kampeni hii iliyowezesha upatikanaji wa fedha pia kampeni hii imeenda sambamba na mafunzo ya walimu 220 ambao wafundishwa namna ya kutoa elimu inayoenda na karne ya 21 ya kuwawezesha wanafunzi wanaohitimu kujitegemea na kuwa viongozi wanaojitambua,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Ameongeza kupitia kampeni ya kuwaweka wanafunzi kambini kwa ajili ya kujisomea wanapokaribia kufanya mitihani ya kidato cha nne, imesaidia kuongeza ufaulu daraja la kwanza kutoka wanafunzi saba hadi 37 na waliopata sifuri kupungua kutoka wanafunzi 257 hadi wanafunzi 175.

Joketi pia ameeleza kuwa sababu ya kufanya kapeni hizo ni kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kufika kidato cha sita ambapo katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2017 jumla ya wanafunzi 4,880 walimaliza kidato cha nne lakini wanafunzi 66 ndio waliofika kidato cha sita.

Wakati huo huo Jokate amepanda mti kwenye eneo ambalo ujenzi wa shule hiyo ya kisasa na ya mfano itajengwa huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Kibuta kwa kukubali kufanyika kwa ujenzi huo ambapo wamekubali kutoa eneo bure.

Amewaomba kuwa bado michango ya wananchi hao inahitajika hasa kwa kuzingatia wakati wa ujenzi kutachimbwa mitaro ,utachimbwa mchanga na maji na kwamba hayo yote yanahitaji nguvu kazi ya wananchi ili kufanikisha ujenzi.

Amewaomba wananchi hao kuendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya hiyo katika kufanikisha jambo hilo jema na lenye tija kwa Wana Kisarawe na Watanzania kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine wananchi wilayani humo wamesema wamefurahishwa na namna ambavyo Mkuu wa Wilaya hiyo ambavyo amekuwa akishirikiana nao katika kufanya maendeleo ambapo wameahidi watatumia muda,nguvu na maarifa yao kufanikisha ujenzi wa shule hiyo unafanikiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad