HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 11 April 2019

BONYOKWA WAANZA KUFURAHIA HUDUMA YA MAJI BAADA YA MIAKA MINGI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAKAZI wa Kata  ya Bonyokwa na vitongoji kwa mara ya kwanza leo wameanza kupata huduma ya maji baada ya kuyakosa kwa kipindi kirefu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao wameonesha furaha ya kupata maji safi na salama baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na huduma hiyo.

Mkazi wa Bonyokwa Athanas Massaka amesema kuwa ni miaka mingi sana hawajawahi kupata maji ya bomba zaidi wamekuwa wanatumia maji ya visima ila kuanzia leo wataanza kutumia maji safi na salama.

Massaka amesema, kazi kubwa imefanywa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa kuwezesha mradi wa maji wa kuja katika Kata yao kwa mara ya kwanza.

Amesema, wanaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuhakikisha wananchi wa pembezoni mwa mji wanapata maji hata itakapofika 2020 watakuwa na cha kujivunia.


Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema  wananchi wa Bonyokwa wataanza kupata maji leo baada ya kukamilika kwa mradi  huo wenye urefu wa Km 3 na utahudumia wananchi 30,000.

Luhemeja amesema, tayari wameshafanya maunganisho mapya ya wateja 1500 ambao wote kwa pamoja wataanza kutumia maji safi na salama na kuwasisitiza wananchi wengine wajitokeze kwenda kwenye ofisi za DAWASA kuweza kupata utaratibu wa kujiunga kwa mkopo.

Luhemeja yupo katik ziara ya wiki moja akitembelea miradi 41 inayosimamiwa na Mamlaka hiyo kwa kutumia fedha za ndani zikiwa kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (aliyenyanyua mikono) akifurahia mara baada ya kutobolewa bomba la maji litakalokuwa likiwasambazia wakazi wa Bonyokwa na Vitongoji vyake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha bomba.
Moja ya bomba lililofungwa kwa wakazi wa Bonyokwa kuendelea kupata maji.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad