HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 11, 2019

DAWASA YAWAAHIDI WANANCHI WA MKURANGA KUPATA MAJI KUFIKIA DESEMBA MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIKA kuhakikisha wananchi wa pembezoni mwa mji wanapata maji safi na salama, Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imedhamiria kuwapelekea maji wananchi wa Mkuranga ifikapo Desemba mwaka huu.DAWASA kwa kutumia fedha za ndani takribani bilion 5.6 wameanza mchakato wa kupeleka mabomba na kuyalaza kwa urefu wa Km 15 kuanzia kwenye mradi huo na kuepelekwa maeneo ya karibu ya Mkuranga..


Akielezea mikakati hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mkandarasi ataingia kazini mwezi Mei mwaka huu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu itakayowezesha kusambaza maji kwa wananchi wa Mkuranga na maeneo ya karibu.

"Mkandarasi ataingia kazini Mwezi Mei mwaka huu, na kuanzia kesho April 12 tutaanza kazi ya ulazaji wa mabomba  yatakayokuwa na urefu kwa Km 15,"amesema Luhemeja.


Luhemeja amesema, mpaka sasa wananchi 2500 ndio wanaopata maji kati ya wananchi 25,500 na wamechimba kisima chenye urefu wa Mita 600 na kutajengwa tenki litakalokuwa na uwezo wa lkuhifadhi maji Lita Milion 1.5 kwa siku.


Amesema, hii ni mikakati ya kufungua maeneo ya pembezoni na mradi huu ukikamilika wananchi wa Mkuranga, Vikindu hadi Mbagala watanufaika kwa kupata maji safi na salama.Mhandisi Luhemeja amewaomba wananchi kuvumilia mpaka Disemba wataanza kupata maji safi na salama ambapo yataondoa kero ya miaka mingi ya kutokuwa na huduma hiyo.

Ziara ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA inaendelea lwenye miradi tofauti ambapo ipo kwenye hatua mbalimbali za umaliziaji na mingine ikiwa hatua za awali kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika hususani pembezoni mwa mji ambapo hakukuwa na mtandao wa maji wa DAWASA.


Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akisikiliza maelezo ya mradi wa Kisima cha Mkuranga, Pwani kutoka kwa Msimamizi wa Mradi Mhandisi John Kirecha (wa pili toka kulia) wakati wa ziara ya kutembelea kujionea maendeleo ya mradi huo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionja maji ya kisima yatakayosambaziwa wakazi wa Mkuranga, Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili toka kushoto) akiendelea kukagua mradi wa kisima kilichopo Mkuranga, Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad