WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefunga soko la wakimbizi na wananchi lililoanzishwa nje ya kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma. Hatua hiyo imekuja baada ya soko hilo kubainika kuwa  chanzo cha  wakimbizi kutoka nje ya kambi kiholela na kushiriki katika kufanya matukio ya kiharifu.
Waziri Mkuu ametangaza uamuzi huo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa umma katika ya Halmashauri ya Kibondo. ”Vitendo vya uhalifu wilayani Kibondo vikiwemo vya utekaji wa watoto vimeongezeka na kusababisha hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.”
Waziri Mkuu amesema ni vema halmashauri hiyo ikaandaa utaratibu wa kutoa vibali vitakavyowaruhusu Watanzania kupeleka bidhaa ndani ya kambi hivyo. Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wananchi waliopewa dhamana ya kufanya kazi kwenye kambi za wakimbizi wawe waadilifu na wasimamie sheria.
“Nafahamu tunao watendaji wetu ambao wapo kambini kusimamia shughuli mbalimbali za wakimbizi,  tekelezeni wajibu wenu ipasavyo na si vinginevyo.” Baada ya kuzungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Kibondo, Waziri Mkuu alikwenda wilayani Kakonko na kukagua mradi wa maji Muhange. Pia Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Kakonko unaotarajiwa kugharimu sh. bilioni 4.5. 
 Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye 
eneo la Mradi wa Maji wa  Muhange wilayani Kakonko kukagua mradi huo, 
Februari 19, 2019. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mbunge wa Buyungu, 
Mhandishi Christopher Chiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke
 wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha 
 Muhange wilayani Kakonko wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokagua
 Mradi wa Maji kijijini hapo, Februari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya 
Waziri Mkuu)
 Waziri
 Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kakagua Mradi 
wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, Februari 19, 2019.  Wengine kutoka 
kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi 
Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel 
Maganga, Mbunge wa Buyungu Mhandisi Christopher Chiza, Mke wa Waziri 
Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, 
Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na 
Biashara, Mhandisi Stella Manyanya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhange wilayani 
Kakonko, Ibrahim Katunzi jumla ya shilingi milioni moja kwa ajili ya 
Mradi wa Maji na Zahanati katika Kata hiyo, Februari  19, 2019. (Picha 
na Ofisi ya Waziri Mkuu)


No comments:
Post a Comment