HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 19, 2019

WARAGHABISHI WAKUTANA DODOMA KWENYE MKUTANO WA DIGITALI NA MAENDELEO

Na Vero Ignatus, Dodoma
Serikali imewapongeza waandishi wa habari za mtandao kwa kufikisha taarifa kwa jamii kwa haraka hali inayopelekea wananchi kuchukua hatua katika kuleta mabadiliko. Akizungumza katika mkutano mkuu wa Waragabishi ulioandaliwa Shirika la Oxfam Tanzania Jijini Dodoma  Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaac Kamwele wakati akitoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa Dijitali kwa maendeleo

Waziri amesema kuwa  Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika matumizi ya mitandao katika mifumo mbalimbali ya shughuli za serikali kila siku ili kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma Bora, umoja na muunganiko wa wananchi uwajibikaji na uwazi ndani ya Serikali uwajibikaji wa wananchi katika maendeleo

Akitoa hotuba kwa  niaba ya makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Mhandisi  Kamwele amesema kuwa Waandishi wa habari za mtandao wana nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko kwani wanawafikia watu wengi kwa muda mchache. Sambamba na hayo ametoa wito kwa wananchi wanaomiliki simu janja kutumia simu zao vizuri katika kuleta mabadiliko kiuchumi na kuacha tabia ya kutumia simu zao kwa mambo yanayovunja maadili katika jamii.

'' Tunazidi kuboresha ili kwamba Mtanzania popote alipo aweze kupata habari hizi , na tumeanzisha mfuko ili kuhakikisha minara sasa inakwenda mpaka vijijini  kwani miundombinu mingi ya mitandao iko mijini''Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Odokorach Francis amesema kuwa Shirika la Oxfam kupitia mradi wa chukuaHatua limefanikiwa kuwamilikisha Ardhi wanawake 300 katika halmashauri za Mbogwe,Shinyanga vijijini,Kishapu na Hanang. Francis amesema Oxfam pia imefanikiwa kuwafikia wanawake wanaoishi maisha duni katika kambi za wakimbizi za kigoma kwa kuwafikishia huduma za maji na huduma zingine muhimu za kijamii

Shirika la Oxfam limejitosa kuwawezesha watetezi wa haki za binadamu katika matumizi ya teknolojia ya digitali ili kupata majibu ya haraka ya changamoto za kijamii na haki za binadamu kutoka kwa viongozi wa serikali

Aidha Oxfam walitoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya digitali kupitia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook na Whatsapp kwa watetezi mbalimbali wa mikoa ya Mtwara, Kigoma , Arusha na Geita ambao wanaitwa (WARAGHBISHI) ili waweze kuleta maendeleo katika jamii zao

'' Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)inashiriki kama mdau muhimu sana katika eneo hili la matumizi ya mitandao ili kutetea haki za binadamu''Alisema

Mkutano huo uliofanyika Dodoma - African Dreams Hotel ambapo watatoa taarifa za mafanikio na changamoto katika matumizi ya  teknolojia ya mtandao katika kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kijamii. Mkutano huo wa  siku mbili  Dijitali kwa maendeleo imejumuisha wadau zaidi ya 150 kutoka mikoa mbali mbali nchini kwa lengo la kujifunza mafanikio ya Dijitali katika kuleta maendeleo.
 Waziri waUjenzi, Uchukuzi nw Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa waraghabishi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Oxfam nchini Tanzania Odokorach Francis akizungumza na waraghabishi zaidi ya 150 waliohudhuria katika mkutano huo leo Jijini Dodoma
 Baadhi ya Waraghabishi kutoka katika mikoa mbalimbali wakiwa katika mkutano katika ukumbi wa African Dream's Jijini Dodoma
 Mbunge wa Mbogwe Geita Augustino Masele akichangia mada katika mkutano wa Digitalikwa maendeleo leo Jijini Dodoma
Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia akiwa anachangia mjadala katika mkutano leo Dodoma
 Mbunge wa Hanang'Mary Nagu akifuatia taarifa kupitia simu yake ya kiganjani
 Baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni wakifuatilia jambo kwa makini  (Picha/ habari na Vero Ignatus ) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad