HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

WAHAMIAJI HARAMU 22 MIKONONI MWA POLISI MKOANI TABORA

Na Amisa Mussa
Jeshi La Polisi Mkoani Tabora Kwa kushirikiana na raia wema limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu  ishirini na wawili ambao walikua wakisafiri kutoka Burundi kupitia Kigoma, Tabora kuelekea nchini Zambia wakiwa kwenye usafiri wa basi  la An.

Miongoni mwa raia hao wa Burundi  waliokamatwa tisa ni watoto wadogo ,ambao walikua pamoja na wazazi wao katika safari yao, raia hao wamekamatwa wakiwa wanaingia kwenye  kituo kikuu cha mabasi Mjini Tabora ndani ya basi  la An ambalo linafanya  safari zake  katika Mikoa ya Tabora na Kigoma

Kamanda wa Polisi Wilaya  ya Tabora Mjini John Mfinanga, ambaye aliongoza  kikosi kazi cha askari Polisi wasaidizi  amesema wamefanikiwa kuwakamata raia hao wa Burundi baada ya kupata taarifa za siri juu ya  ujio wao  ambao walikua wakipita hapa Mkoani  Tabora wakielekea nchini Zambia.

baadhi ya wananchi wameviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria mawakala ambao wanawasafirisha  wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad