HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAWASHIKILIA RAIA 10 WA ETHIOPIA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

*Wengine  washikiliwa kwa tuhuma za ubakaji na kupatikana na mali za wizi

JESHI la polisi Mkoani Mbeya linawashikilia raia 10 wa Ethipia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kuwa na kibali maalumu na hiyo ni baada ya msako uliofanywa na jeshi la polisi tarehe 19 mwezi huu  katika kijiji cha Lugelele Wilaya ya Mbarali katika barabara ya itokeayo Njombe kuelekea Mbeya wakiwa wanatembea kwa miguu pasipokuwa na vibali maalumu vya kuishi nchini.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi Mkoani humo Charles Kakola (30) mkazi wa Iwindi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka mitatu ambapo imeelezwa kuwa mtuhumiwa akitekeleza hayo mara baada ya kulewa na mtuhumiwa  amekiri kosa hilo na uchunguzi unaendelea.

Pia katika tukio jingine la ubakaji Samwel Msukila (22) mkazi wa Kilasiro anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka tisa na hadi sasa mama wa mtuhumiwa huyo amekamatwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Katika tukio jingine la ubakaji lililotokea Mbeya vijijini  Alinani Mwakifuna (59) ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwaselela anashikiliwa na jeshi lapolisi kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 15 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni tama za kingono, imeelezwa kuwa mtuhumiwa alimrubuni binti kabla ya kumwingilia kimwili.
 Pia jeshi la polisi Mkoani humo Mkoani humo linawashilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo, kukutwa na mali zinazosadikika kuwa za wizi, kukutwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini pamoja na makosa ya kuingiza bidhaa nchini  bila kuwa na kibali na watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi huku uchunguzi ukiendelea.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad