HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

MWILI WA MENEJA HABARI, MAWASILIANO TFS KUAGWA KESHO DAR

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWILI wa marehemu Glory Mziray ambaye enzi za uhai wake alikuwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) unatarajiwa kuagwa kesho Alhamisi katika Kanisa la KKKT Tanki Bovu jijini Dar es Salaam kuanzia saa sita mchana.

Glory alifikwa na umauti jana saa saba mchana akiwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbambali vya habari nchini katika Ofisi za Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo linajulikana zaidi kwa jina la Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo, TFS inaeleza kuwa mwili wa marehemu Glory leo utapelekwa na kulala nyumbani kwake Goba-Kinzudi na kesho Alhamisi utaagwa katika Kanisa la KKKT Tanki Bovu jijini Dar es Salaam na baada ya hapo atasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Ijumaa baada ya chakula cha mchana.

Taarifa ya TFS imefafanua zaidi kuhusu ratiba hiyo kwa leo inaonesha kwamba waombolezaji wameanza kuwasili nyumbani kwa marehemu Kinzudi saa tatu asubuhi na itakapofika saa 09:30 alasili mwili utawasili nyumbani hapo na kisha kufuatiwa na ibada itakayoanza saa 11 jioni.

Pia kwa kesho Alhamisi ratiba inaonesha waombolezaji wataanza kuwasili saa mbili asubuhi na itakapofika saa nne asubuhi chakula na saa sita ibada ya kuaga(KKKT Tanki Bovu) ikifuatiwa na kutoa heshima za mwisho saa 7:15 mchana.Kwa mujibu wa ratiba hiyo safari ya kuelekea Morogoro itaanza saa 8:00 mchana.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa Ijumaa ya Februari 22, 2019 , inaonesha 02:30 itakuwa ni kifungua kinywa, saa sita chakula cha mchana na saa nane mchana itafanyika ibada ya mazishi ikifuatiwa na kuweka mashada na salamu za makundi maalum.

NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Kwa mujibu wa TFS ni kwamba kwa waombolezaji wanaotaka kufika, Kinzudi ipo katikati ya Salasala na Goba.Njia zipo mbili moja ingia Mmbuyuni elekea njia ya Kinzudi, pia kuna mabasi unashuka Kinzudi Stand kisha unachukua bajaji au bodaboda ambaye itakupeleka Mendeleo street.

Pia unaweza kuingia njia ya Masana halafu unashuka kituo kinaitwa njia panda ya Kata, baada ya hapo chukua bodaboda ikupeleke Maendeleo street ndipo msiba ulipo.Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu ya mkononi katika namba 

0786670454(baba June Amini) au Dk.Martin 0620488216, 0714529562.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad